Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SAKATA LA NGASA LATINGA FIFA

Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umesema unatarajia kujipanga kupeleka malalamiko yao katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ili kupinga adhabu ya kufungiwa mechi sita na kuilipa Simba Sh. milioni 45 ambayo amepewa mshambuliaji wake mpya, Mrisho Ngasa (Pichani).


Hata hivyo, Ngasa tayari ameshaanza kuitumikia adhabu hiyo na tangu Agosti 23 mwaka huu Yanga ilipowasilisha rufaa yake ya kupinga maamuzi hayo haijajibiwa chochote na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF); ambalo kanuni zake zinasema kwamba Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ndiyo ya mwisho katika suala la usajili wa wachezaji.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema kwamba klabu yake inapinga adhabu hiyo kwa kuzingatia kanuni za FIFA za usajili ambazo zinakataza klabu kuingia mkataba na mchezaji ambaye bado hajamaliza mkataba na timu nyingine.

Mwalusako alisema kuwa kipengele 3 (f) cha FIFA kinachohusiana na Hadhi za Wachezaji kinaeleza kwamba kuna vipindi viwili vya usajili na kwa sababu hiyo, wanahoji kuwa je;  Simba ilimsajil Ngasa wakati gani ilhali alikuwa bado ana mkataba na Azam?

Alisema vilevile kuwa kamati hiyo iliyomuadhibu Ngasa haikumtendea haki kwa kutomuita na kumsikiliza hali ya kuwa awali mshambuliaji huyo mwaka jana alionyesha wazi mapenzi  yake kwa Yanga licha ya kuitumikia Azam wakati huo na kuna wakati klabu hiyo ilitangaza kukasirishwa na jambo hilo na kilichofuatia ni mchezaji kuhamishiwa Simba kwa mkopo.

“Ngassa hakuitwa, alinyimwa haki ya msingi ya kusikilizwa na kamati ili kuthibitisha kuhusu tuhuma za kupokea fedha kabla ya kuamua kumpa adhabu kali kama hiyo," alisema Mwalusako.

Aliongeza kwamba wanaamini Simba ilitumia mbinu ya kumrubuni na kumshawishi asaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo nje ya utaratibu wa usajili na wao wanashangaa kuona klabu hiyo (Simba) kutoadhibiwa kwa kosa hilo la kikanuni.

"Kitendo cha kumfungia Ngasa mechi sita ni kuiadhibu klabu ya Yanga kwa kosa ambalo haijahusika nalo.

Yanga imemsajili mchezaji huyu kihalali na ndiyo maana amepitishwa kuichezea timu hii msimu huu," alieleza. Aliongeza kwamba wanashangaa kuona mchezaji huyo akifungiwa kuichezea Yanga na shirikisho hilo kupitia kocha mkuu wa timu ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen, ikimuita kwa ajili ya kwenda kuitumikia nchi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC