Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ROONEY KUNG'OKA MAN UNITED MASAA 48 AMA SIVYO.........

KOCHA Jose Mourinho amempa Wayne Rooney (Pichani0 saa 48 kutangaza hadharani nia ya kuondoka Manchester United kuhamia Chelsea.


Kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Old Trafford jana, kocha huyo wa Chelsea amemuambia mchezaji huyo ‘aliyeanzisha hadithi hiyo’ kwamba sasa ‘anatakiwa kuimalizia’.

Chelsea imekwishapeleka mezani ofa mbili kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa England na iatuma ofa ya tatu ikiwa Rooney atatangaza kuondoka.

Mashabiki wa United waliimba jina la Rooney wakati wa mchezo na Mourinho akasema anataka kupeleka ofa nyingine.

Kocha huyo Chelsea amesema: "Hatkuanzisha hii habari. Mtu fulani alianzisha habari hiyo kwa kusema wazi , nataka kwenda Chelsea, sitaki kubaki Manchester United.

"Sisi si machizi kutafuta wachezaji wazuri ambao wanasema wanafurahia katika klabu zao, lakini nafikiri anatakiwa kusema nataka kuondoka, au nataka kubaki,".

Mourinho baadaye akaweka sawa: "Mtu ambaye alianzisha habari hii anatakiwa kuimaliza. Nataka yeye aseme kama anataka kubaki au kuondoka. Klabu kama yetu, kocha kama mimi na watu ninaofanya nao kazi si wajinga,".

"Tuna saa 24 hadi 48 kufunga huu mjadala au kuendelea nao. Tunajaribu kupata mchezaji kutoka timu kubwa na hawataki kumuuza.

Tusingeweza kumtafuta mtu ikiwa hakuanzisha. Ni wakati wa kufanya maamuzi. Ni mwanasoka kweli, amejaribu kushinda, kufunga, alikuwa babu kubwa.

"Baada ya hiyo ikiwa anataka kuondoka, anatakiwa kusema. Ikiwa hataki kuondoka tena, tutaheshimu hilo na tutasema asante na kuendelea,".
Support: Rooney was cheered by both sets of fans during the match
Sapoti: Rooney alishangilia na mashabiki wa timu zote mbili katika mchezo wa jana

"Alicheza vizuri mechi katika mazingira magumu. Alimuambia mtu mmoja wa karibu yake kwamba ni muhimu anataka kuondoka. Wachezaji wengi katika mazingira kama haya, hawawezi kujipambanua uwanjani. Ameweza, alikuwa bora,".

Mourinho atamsaini Samuel Eto’o kutoka Anzhi Makhachkala kwa bei poa ikiwa atamkosa Rooney. Na hilo ndilo linatazamiwa zaidi baada ya usiku wa jana Rooney kuonyesha kiwango akiwa na jezi ya United Uwanja wa Old Trafford.

Moyes anaamini Rooney tayari amejifunga na United na amemuonya Mourinho kutofanya mambo kinyume cha sheria, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mshambuliaji huyo.

Kocha huyo wa United alisema: "Itakuwa ni uvunjaji wa sheria, hawezi kufanya hivyo,".

"Nimevutiwa sana na kiwango chake na namna mashabiki wote walivyompokea. Haikutarajiwa.

Napaswa kusema, alikuwa babu kubwa mazoezini, kwa namna alivyojifua na alionekana makini sana.

"Fikra zilikuwa kwamba nitakwenda kumchezesha kwa dakika dakika 60 au 70, lakini alishuka hadi chini na kuchukua mipira hadi kwa kuwapokonya miguuni akiitelezea. Nafikiri Wayne ana mawazo sahihi, hayatakiwi kubadilika. Nafikiri kwa sasa, kiwango chake kinaongea kiasi cha kutosha, aliwaacha watu wawili au watatu kwenye kona na umati ulikubali kazi yake aliyofanya. Alikosa kufunga tu, alikaribia kufunga kwa tik tak,"alisema Moyes.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC