Ruka hadi kwenye maudhui makuu

COASTAL UNION WAAPA KUIVURUGIA YANGA KESHO

Huku timu zao zikiwa zimeshinda mechi za kwanza za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, kocha wa Yanga, Ernie Brandts amesema kuwa kikosi chake kina uwezo wa kushinda mechi ya kesho huku kocha Hemed Morocco wa Coastal Union (Pichani) ya jijini Tanga akitamba 'kuwavurugia' mabingwa hao watetezi.


Yanga ilianza ligi kwa ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Ashanti United wakati Coastal Union iliyosukwa upya ilishinda 2-0 dhidi ya JKT Mgambo ugenini Arusha Jumamosi.

Akizungumza jana, Brandts alisema kuwa timu yake imejiandaa kukabiliana na ushindani kutoka katika timu zote hivyo hawatarajii kupoteza mechi hiyo ya raundi ya pili itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Brandts alisema kwamba anajua mechi hiyo itakuwa na ushindani kwa sababu wapinzani wao wamefanya mabadiliko katika kikosi chao na wana morali baada ya ushindi wa mechi yao ya ufunguzi.
Mholanzi huyo alisema kwamba timu yake iko katika hali nzuri na watatumia faida ya uwanja wa nyumbani kuwakabili wapinzani wao.

Morocco ambaye waliwasili jijini juzi usiku amewataka mashabiki wa timu hiyo kujiandaa kuona soka la kisasa ambalo lengo lake ni kushinda na kutoa burudani.

Alisema kwamba hawaidharau Yanga na anafahamu ni wachezaji gani 'hatari' wanafaa kuzuiwa (hakuwataja majina) ili kuwadhibiti katika mechi hiyo.

"Najua nani anafaa kutulizwa na njia zipi za kuzuia ili kuvuruga mipango yao," aliongeza Morocco, ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Zanzibar Heroes.

Alimtaja mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars), Crispin Odulla na Daniel Lyanga kuwa ndio nyota watakaoongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Bara mwaka 1988.

Alisema pia nyota wa zamani wa Simba ambao wametua kwenye kikosi hicho, Juma Nyosso, Uhuru Suleiman na Haruna Moshi ' Boban' wanatarajia kuisaidia timu yake kupata ushindi hapo kesho.

Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, aliwataja wachezaji ambao wametoka kuwa majeruhi na wanafanya mazoezi mepesi kuwa ni pamoja na Kelvin Yondani, Athumani Iddi 'Chuji' na Ibrahim Job.

Baada ya mechi za kesho kumalizika, ligi hiyo itasimama kupisha kambi ya timu ya Tanzania (Taifa Stars) itakayoanza keshokutwa ili kujiandaa na mechi ya kukamilisha ratiba ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Gambia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC