Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TPBO, PST WALUMBANA KUMGOMBEA CHEKA, MWENYEWE AFURAHIA


Kitendo cha bondia Francis ‘SMG’ Cheka (Pichani) kusaini mkataba wa kupigana na mmalawi, Chiotcha Chimwemwe kimeibua ‘bifu’ baina ya viongozi wawili wa vyama vya ngumi za kulipwa Tanzania vya TPBO Limited na PST.

TPBO na PST zimeingia kwenye mgogoro huo kufuatia PST kutoa kibali kwa Cheka cha kupigana na Chimwemwe, wakati ikijua TPBO pia imetoa kibali kwa bondia huyo kupigana mwezi huo na Mmarekani.
Rais wa TPBO, Yassin Abdallah alimtuhumu mwenzake wa PST, Emmanuel Mlundwa kwa kumpa kibali Cheka kupigana na Chimwemwe Agosti 10, wakati akiwa amesaini kucheza na Derrick Findley wa Marekani siku 20 baadaye.
Malumbano hayo yalianza baada ya Abdallah kumtaja Mlundwa kama kiongozi wa masilahi ambaye anawatumia mabondia kama matrekta yake ili kujiingizia kipato huku akitolea mifano mapambano kadhaa yaliyowahi kusimamiwa na PST.
Wakati Mlundwa akimjibu Abdallah kwa kumwambia kuwa anataka kujidai anajua ngumi wakati hata gloves hajawahi kuvaa na kufananisha maneno yake na ujinga.
Vyama vya ngumi za kulipwa nchini vimekuwa kwenye migogoro ya mara kwa mara ya utoaji vibali vya mapambano ya mabondia, ambapo PST iliwahi kuingia kwenye mgogoro na TPBC kufuatia TPBC kutoa kibali kwa Karama Nyilawila kupigana na Cheka wakati akitakiwa kutetea ubingwa wake wa dunia.
Hata hivyo Cheka ambaye sasa yuko kambini jijini Nairobi, Kenya amebainisha kuwa anaweza kucheza mapambano yote mawili kwa mwezi Agosti.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC