RT KUJADILI KATIBA YAO JULAI 27 MORO

WAKATI Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), likiwa limekamilisha rasimu ya katiba yake, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo inatarajiwa kukutana Julai 27 mjini Morogoro kwa ajili ya kuipitia kabla ya kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui(Pichani, alisema katiba ya shirikisho hilo imekamilika na tayari wameisambaza kwa wajumbe wote wa kamati ya utendaji.

“Tumekamilisha katiba ya chama, Julai 27; tutakutana na Kamati ya Utendaji, pamoja na wadau kwa ajili ya kujadili na kupitisha katiba hiyo, ambayo itaanza kutumika baada ya kupata baraka za mkutano mkuu,” alisema Nyambui.

Mbali na katiba, Nyambui alisema, wako katika maandalizi ya mashinndano ya taifa ambayo yanatarajia kufanyika Agosti 23 na 24 na kufuatiwa na mkutano mkuu wa kupitisha rasimu ya katiba Julai 25 mjini Morogoro.

Alisema, licha ya kukabiliwa na ukata, wanaendelea na maandalizi ya mashindano hayo pamoja maandalizi ya mashindano ya dunia, ambayo Tanzania itawakilishwa na wanariadha watatu.

Nyambui aliziomba kampuni na tasisi za serikali na binafsi, kujitokeza kudhamini mashindano hayo, kwani hadi sasa hakuna mdhamini aliyejitokeza.

“Timu ambazo zitashiriki mashindano ya taifa, zinatakiwa zithibitishe mwanzoni mwa mwezi ujao na wanariadha ambao watashiriki mashindano ya dunia huko Moscow, Urusi wako kambini jijini Arusha wanaendelea na mazoezi,” alisema Nyambui.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI