Ruka hadi kwenye maudhui makuu

RODGERS KUMBAKISHA SUAREZ LIVERPOOL

Brendan Rodgers

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anatarajia Luis Suarez asalie katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao lakini hajafutilia mbali uwezekano kwamba straika huyo wa Uruguay huenda akauzwa kwa bei ifaayo.

Suarez, aliyeibuka wa pili kwa ufungaji mabao Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na mabao 23 msimu uliopita, alisema anataka kuondoka Liverpool akacheze soka Uhispania, akilaumu vyombo vya habari vya Uingereza kwa kufanya maisha yake yawe magumu Uingereza.
Licha ya uvumi mwingi kuhusu siku zake za usoni, mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 amejiunga na wachezaji wenzake Australia kwa mechi ya kabla ya msimu Jumatano dhidi ya Melbourne Victory.
"Ndio, kabisa,” Rodgers aliambia wanahabari mjini Melbourne mnamo Jumatatu alipoulizwa ikiwa anatarajia Suarez aendelee kukaa Liverpool.
"Ni mchezaji ambaye kwa kweli amezungumziwa sawa na kumwekuwa na uvumi mwingi kipindi hiki cha nje ya msimu.
"Lakini ukweli ni kwamba ni mchezaji anayethaminiwa sana Liverpool.
"Labda kuwe na ofa yoyote ambayo itakaribia thamani yake na kwa sasa hakuna lolote la kujadili kwani hatujakuwa nayo.
“Kwa hivyo, kwa sasa, ako nasi, amejiunga nasi na anafaa kuanza mazoezi wakati ufaao.
“Amepumzika vya kutosha na anasubiri kwa hamu na ghamu kuwa tayari kwa mchezo pamoja na timu.”
Alipoulizwa kuhusu ofa ambayo inaweza kushawishi klabu hiyo, Rodgers alijibu: "Sikusema tutamuuza. Nilisema kila mchezaji ana thamani na bei. Haimaniishi kwamba lazima auzwe.”
Suarez, aliyejiunga na timu hiyo kutoka Ajax Amsterdam Januari 2011, ametia ila ustadi wake uwanjani na visa vya utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na marufuku ya mechi 10 kwa kumuuma Branislav Ivanovic wa Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita.
Hiyo ilifuatia marufuku nyingine ya mechi nane msimu uliotangulia na ukosoaji mkali kutokana na matamshi ya ubaguzi wa rangi.
Suarez aliwasili Australia kabla ya wenzake, waliolaza Indonesian XI 2-0 mjini Jakarta Jumamosi usiku, baada ya kupewa muda wa ziada wa kupumzika baada yake kucheza Kombe la Confederations.
Rodgers alisema ana “furaha sana” na huenda acheze kwenye mechi ya Jumatano dhidi ya Victory uwanja wa Melbourne Cricket Ground, ambapo mashabiki zaidi ya 90 000 wanatarajiwa kufika kujionea mechi.
Kocha huyo bado hajaketi kwa mazungumzo na Suarez kujua msimamo wake, hata hivyo.
“Sijakuwa na kikao naye bao,” Rodgers akasema. “Tuliwasili tu usiku.”
"Bila shaka aliwasili hapa kabla yetu akitokea sehemu tofauti ya dunia lakini kama ambavyo tumekuwa daima kama klabu na bila shaka kama meneja na kocha sina wasiwashi kuhusu hilo.
"Luis yuko hapa kama alivyotarajiwa. Ni sehemu kuu ya timu yetu. Tutaketi na kuzungumza wakati mmoja na huwa nafanya hivyo na wachezaji wote.
"Atajiunga na mazoezi leo na wachezaji wengine wote na katika kipindi cha wiki chache zijazo tutawasiliana naye na nimekuwa nikiwasiliana naye msimu wote wa majira ya joto.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC