Ruka hadi kwenye maudhui makuu

OWINO AIBUKIA ULINZI YA KENYA



Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya mwaka 2010 (KPL) Ulinzi Stars wameteua kikosi kikali cha wachezaji 20 kinachochanganya ujana na ujuzi kwa ajili ya Michezo ya Wanajeshi Afrika Mashariki itakayoandaliwa Nairobi wiki ijayo.

Nahodha Evans Amuoka ataongoza kikosi hicho ambacho pia kinajumuisha mchezaji aliyejiunga nao majuzi Fred Chitai na kipa asiyejulikana sana Fineas Odhiambo.
Hayo yanajiri chini ya wiki tatu baada ya wanajeshi hao kushiriki Michezo ya Wanajeshi ya Dunia mjini Baku, Azerbaijan ambapo walishindwa kufuzu kutoka ngazi ya makundi. Lakini ushindi wao mara mbili hivi majuzi kwenye ligi ya nyumbani dhidi ya Chemelil Sugar na Nairobi City Stars unawapa motisha wanapoelekea kwenye dimba hilo.
Kwa mujibu wa mkuu wa timu hiyo Meja Erick Oloo, timu hiyo iko tayari kupigania taji ambalo walipoza pembamba kwa Uganda mwaka uliopita nchini Rwanda.
“Tuko tayari wakati huu kushinda taji. Kuwa wenyeji wakati huu pia kutatufaa zaidi na tunalenga kushinda. Mwaka uliopita, Uganda walitushinda kwa wingi wa mabao lakini tunawaambia watarajie kibarua wakati huu,” Meja Oloo aliambia tovuti rasmi ya klabu hiyo.
Baada ya mechi ya ligi Jumamosi dhidi ya AFC Leopards, klabu hiyo yenye makao yake Nakuru itapewa ruhusa kwenda kushiriki dimba hilo la eneo la Afrika Mashariki.
“Baada ya mechi dhidi ya AFC Leopards mnamo Jumamosi, tutaingia kambini kujiandaa kwa michezo hiyo na mechi itakayofuata ya KPL ambayo itakuwa Agosti 14 dhidi ya Karuturi mjini Naivasha,” akaongeza Meja Oloo.
Kikosi: Francis Ochieng, Franklyn Miheso, Fineas Odhiambo, Fred Chitai, Mohammed Hassan, Mulinge Ndetto, Geoffrey Kokoyo, Josiah Okello, Oliver Kiprutto, Amon Mwamburi, Mohammed Abulala,Stephen Ochollah,Antony Muriithi, Collins Ochieng, Lawrence Owino, Kelvin Amwayi, Salim Mohammed, Oliver Agwanda, Evans Amwoka na Stephen Waruru.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC