Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KOCHA YANGA AWACHIMBA MKWARA NYOTA WAPYA

Benchi la ufundi la Yanga limewataka wachezaji wapya wa timu hiyo kuonysha uwezo wao mazoezini ili kumshawishi kocha kuwapa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo badala ya kutegemea mtelemko kwenye kupata namba kwa sababu tu ni wapya.

Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Fred Felix 'Minziro' (Pichani) alisema timu imefanya usajili wa wachezaji wapya lakini wachezaji hao hawajahakikishiwa namba ya kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
"Ukiangalia ushindani mkubwa upo kwenye safu ya ushambuliaji kwa sababu Javu (Hussein) ameongezeka," alisema Minziro.
"Lakini hii ni changamoto kwa wachezaji wote wapya na hata wale waliokuwepo msimu uliopita kuhakikisha wanajituma ili kupata nafasi."
Alisema makocha hawataangalia jina la mchezaji bali uwezo wake ambao ndiyo utakaompa namba kwenye kikosi cha kwanza.
Alisema kila mchezaji ana nafasi sawa ya kucheza isipokuwa juhudi na kujituma kwake ndiyo "tiketi" yake ya kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.
Kusajaliwa kwa Javu kunafanya kikosi cha Yanga kuwa na wachezaji sita wa nafasi ya ushambuliaji.
Wachezaji hao mbali na Javu ni Said Bahanuzi, Jerry Tegete, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa ambaye hata hivyo kocha Ernest Brandts anaweza akamtumia kama winga na Hamis Kiiza ambaye inasemekana Yanga imeamua kumuongeza mkataba hatimaye.
Yanga itafungua pazia la ligi kuu ya Bara msimu ujao kwa kucheza na Ashanti United Agosti 24 kwenye Uwanja wa Taifa lakini wiki moja kabla ya mechi hiyo itacheza na Azam kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC