Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KLABU LIGI KUU ZAPONDA RATIBA, ZADAI AZAM IMEBEBWA

Mkurugenzi wa Coastal Union, Nassor Binslum
Baadhi ya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zimeponda vikali ratiba ya ligi hiyo msimu ujao wa 2013/2014 iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kudai kuwa imejaa kasoro nyingi za kiufundi ikiwa ni pamoja na kuonekana ikizipa unafuu baadhi ya timu ikiwamo ya Azam.


Mojawapo ya timu zinazolalamikia ligi hiyo ni Coastal Union ya Tanga iliyowahi kutwaa ubingwa wa Bara mwaka 1988, ikida kwamba ratiba ya msimu ujao unaoanza Agosti 24 'inawaumiza' wao na kuwabeba baadhi ya mahasimu wao.

Akizungumza  jana, Mkurugenzi wa Coastal Union, Nassor Binslum, alisema kuwa anashangaa kuona kuwa katika msimu wa tatu mfululizo tangu warejee katika ligi hiyo wakiendelea kupangiwa ratiba inayoonyesha kuwa wanaanzia nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Mkwakwani kuzikabili Simba na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza na kumalizia ugenini na wapinzani hao hao.

Binslum alisema kuwa ratiba hiyo pia inaonyesha baadhi ya timu kama mabingwa watetezi, Yanga, wakicheza mechi zao zote mbili jijini Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya City wakati wao (Coastal) wakilazimika kusafiri mara mbili kwenda Mbeya kuzikabili timu hizo.

"Nashangazwa na upangaji huu. Sisi tunakwenda Mbeya kucheza na Mbeya City mzunguko wa kwanza halafu raundi ya pili pia tufunge safari ya kucheza na Prisons... sasa sijui kama ni sawa katika taratibu za kupanga ratiba au vipi," alihoji kiongozi huyo.

Kiongozi mmoja wa JKT Ruvu alikaririwa juzi kupitia luninga akilalamika kuwa ratiba hiyo imewaumiza wao katika baadhi ya mechi kwa kuwapangia katika siku zilizokaribiana sana na hivyo kuwapa muda mfupi tu wa kupumzika.

Kocha wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa, alisema kuwa baadhi ya mechi zao kwenye ratiba hiyo zinaonyesha kuwa ni kama imekopiwa ya miaka iliyopita, lakini kwa ujumla haoni kama ina tatizo kubwa kama itafuatwa.

"Mechi yetu dhidi ya Prisons imekaa vile vile kama ilivyokuwa msimu uliopita... ila tunaona (ratiba) imezingatia muda wa timu kusafiri kwa kuondoa mechi za Jumatatu," alisema kocha huyo.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Saad Kawemba, aliwataka viongozi wa timu zote ambazo zinahisi kuumizwa kutokana na ratiba hiyo kuwasilisha hoja zao kwa maandishi mapema ili zifanyiwe kazi na kuondoa kasoro zitakazobainika kabla ya ligi hiyo kuanza.

Kawemba alisema kwamba watakapogundua kuwa kweli kuna matatizo ya msingi katika ratiba hiyo, kamwe hawatasita kuirekebisha.

"Ni kweli kwamba baadhi ya timu zinaonekana zikicheza mechi nyingi Dar es Salaam na nyingine za ugenini ... hii inatokana na ukweli kuwa Dar ina timu sita na kamati yake ilitaka timu itakayoanzia kwenda Kagera kucheza dhidi ya Kagera Sugar basi iende pia Tabora kumalizana na Rhino Rangers... lakini miundombinu pia ni kikwazo kikubwa na imefikiriwa wakati wa upangaji ratiba," alieleza Kawemba.

Ligi hiyo itakayomalizika April 27, 2014 ndiyo ya juu kwa ngazi ya klabu Tanzania Bara na pia ndiyo inayotoa wawakilishi wa Bara katika michuano ya klabu ya kimataifa ikiwamo ya ligi ya klabu bingwa na Kombe la Shirikisho.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...