Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KIBADEN AIHOFIA RHINO RANGERS, ADAI ITAWAKAMIA

Kocha wa klabu ya Simba, Abdallah Kibadeni (Pichani), amesema kupangwa kufungua dimba la msimu mpya wa ligi kuu ya Bara dhidi ya Rhino Rangers iliyopanda daraja ni mechi ngumu kwake kwa sababu timu ngeni huwa na kawaida ya kupania.

Akizungumza jana, Kibadeni alisema katika kuhakikisha timu yake inakuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Rhino, Simba itacheza mechi nne zaidi za kirafiki ikiwemo ya leo dhidi ya Coastal Union, mjini Tanga.
Simba itacheza na Rhino Rangers kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mjini Tabora Agosti 24 na Kibadeni amesema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa Rhino Rangers watataka kuonyesha umwamba wake baada ya kupanda daraja.
Alisema kuwa kwa kuanzia Simba leo wanashuka kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kucheza na Coastal Union kwenye mchezo wa kirafiki.
Kocha huyo wa Simba amesema mchezo huo ni kati ya mchezo minne ya kirafiki aliyopanga kucheza kabla ya kuanza kwa ligi kuu.
"Kupangwa kuanza na timu ngeni kwenye ligi mara nyingi mchezo unakuwa mgumu kwa sababu naamini Rhino Rangers watatukamia," alisema Kibadeni.
Kibadeni amerudi kufundisha Simba baada ya kuwa kocha bora wa mwaka jana alipoiwezesha Kagera Sugar kushika nafasi ya nne kwenye ligi kuu ya Bara licha ya udogo wa timu hiyo ya Bukoba.
"Tunaendelea na maandalizi michezo (na) minne au mitatu ya kirafiki itatuweka vizuri kuwakabili Rhino kwenye ligi," alisema Kibadeni.
Alisema kuwa baada ya mchezo huo wa leo dhidi ya Coastal Union, Simba itacheza micheo mingine miwili kabla ya kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki kwenye kilele cha Siku ya Simba 'Simba Day' Agosti 8 mwaka huu.
Akizungumzia kikosi chake, Kibadeni alisema tayari amepata timu ya kwanza na kwa sasa anakazania mfumo atakaokuwa akiutumia kwenye ligi.
"Kikosi changu kipo tayari na mimi kama kocha najua kikosi changu cha kwanza," alisema Kibadeni na kueleza zaidi:
"Kwa sasa kikubwa ninachokifanya ni kuwazoesha mfumo ninaotaka kuutumia kwenye ligi na mashindano mengine."
Alisema hatakuwa na mfumo mmoja, hata hivyo, bali ameandaa mifumo mitatu atakayokuwa akiitumia kulingana na mbinu za timu wanayocheza nayo.
Mchezo dhidi ya Coastal Union utakuwa wa kwanza wa Simba tangu kupata kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa URA ya Uganda kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wiki mbili zilizopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC