Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BREKING NEWS: HAMISI KIIZA HUYOOOO COASTAL UNION.......

Coastal Union ya Tanga, imeendelea na dhamira yake ya kuvibomoa vigogo vya soka nchini, baada ya juzi kupiga hodi Yanga wakitaka kumsajili mshambuliaji asiyetulia Jangwani, Mganda Hamis Kiiza (Pichani).
Union imekuwa ikifuatilia kwa karibu mzozo wa kimasilahi kati ya Kiiza na uongozi wa Yanga, kabla ya mwanzoni mwa wiki kufikia uamuzi wa kuweka mezani Dola 25,000 ili kumchomoa nyota huyo.
Kama hatua hiyo itafanikiwa, basi Kiiza ataungana na wachezaji wengine watatu waliosajiliwa na Coastal, Haruna Moshi ‘Boban’, Juma Nyoso kutoka Simba na Uhuru Seleman aliyekuwa akicheza kwa mkopo Azam FC.
Kiiza, aliyekuwa kiini cha mafanikio Jangwani msimu uliopita hata kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Bara, hajasaini mkataba mpya kwa kile kilichoelezwa kutaka dau kubwa kuliko uwezo wa Yanga.
Akizungumza jana, kiongozi mmoja wa Coastal Union ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji, alikiri kuwepo mpango huo.
“Ni kweli, tumepeleka ofa Jangwani kutaka kumsajili Kiiza, na kinachoendelea sasa ni kufanya mazungumzo na mchezaji huyo ili tujue hatima ya baadaye,” alisema kiongozi huyo.
“Tunajua Kiiza ni mchezaji mzuri, na dau lake lazima liwe nzuri. Hatuna shaka na uwezo wake, tuko tayari kutoa dola 25,000 (Sh39.5 milioni) ili aje kucheza Uwanja wa Mkwakwani,” aliongeza.
Mapema wiki iliyopita Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga Abdallah Binkleb, alikaririwa akisema kutokuwapo uwezekano wowote wa klabu hiyo kumpiga bei Kiiza.
“Tunamuhitaji Kiiza, ni mchezaji mzuri na bado mchango wake unatakiwa. Hatuwezi na wala hatuna mpango wa kumuuza kwa sasa pamoja na kutaka dau kubwa ili abaki,” alisema Binkleb.
Kiiza amegoma kusajili Yanga akitaka kulipwa Dola 40,000 (Sh63.2 milioni). Lakini uongozi wa Yanga umemtaka kuchukua Dola 35,000 (Sh55 milioni) na kiasi cha Dola 5,000 (Sh7.9 milioni) anunuliwe gari, uamuzi aliopinga mchezaji huyo.
Klabu ya nchini kwake Uganda, URA nayo ilielezwa kuwa tayari kutoa Dola 40,000 ambazo Yanga wanashindwa kumpa Kiiza na mshahara wa mwezi Dola 1,000 ili arudi kucheza Ligi ya Uganda.
Kwa upande wa msemaji wa Coastal, Eddo Kumwembe alithibitisha klabu hiyo kutuma maombi ya kumsajili Kiiza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC