Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BARCELONA YAMTANGAZA GERARDO MARTINO KUWA KOCHA MPYA, SASA KUENDELEZA PASI ZA VILANOVA

Sanpped: Martino, pictured this week, has clinched a two-year deal at the Nou CampKLABU ya Barcelona imefikia makubaliano na Muargentina, Gerardo Martino (Pichani) kuwa kocha wao mpya.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50, ambaye aliiongoza Old Boys ya Newell kutwaa taji la Clausura Argnetina msimu uliopita, amekubali Mkataba wa miaka wa miaka miwili Barca ambako anakwenda kurithi mikoba ya Tito Vilanova.
Barca ilitangaza Ijumaa usiku kwamba, Vilanova mwenye umri wa miaka 44 amejiuzulu ili kuendelea kupata matibabu ya saratani.
New man: Barcelona have sealed a deal to make Gerardo Martino their new manager
Mtu mpya: Barcelona  imemchukua Gerardo Martino kuwa kocha wao mpya
Stepping down: Tito Vilanova resigned from the Barca manager's post due to his continuing battle with cancer
Ameachia ngazi: Tito Vilanova amejiuzulu Barca ili kuendelea kupata tiba ya saratani

"FC Barcelona imefikia makubaliano na kumteua Gerardo Martino kuwa kocha mpya wa timu ya soka kwa misimu miwili ijayo. Makubaliano hayo yanafutiwa na utayarishaji wa Mkataba na kusaini,"imesema taarifa kwenye fcbarcelona.cat read.
"Saa zijazo [mipango ilivyo] akiwasili Barcelona, atasaini Mkataba na kutambulishwa mara,".
Makocha kadhaa wazawa walitabiriwa kupewa kazi na mabingwa hao wa Hispania, wakiwemo Luis Enrique, Andre Villas-Boas, Marcelo Bielsa, Michael Laudrup na Guus Hiddink, ambaye jana amejiuzulu Anzhi Makhachkala.
Kindred spirits: Martino is from Rosario in Argentina, like Barcelona's talisman Lionel Messi
Kocha wa nyumbani: Martino anatokea Rosario nchini Argentina, kama mfalme wa mabao wa Barcelona, Lionel Messi

Pamoja na hayo, Martino aliwapiku wote hao na kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Argentina, amethibitishwa leo kuwa kocha mpya.
Martino amekuwa kocha wa timu ya Newell ya nyumbani kwao, Rosario kwa misimu miwili iliyopita na aliichezea klabu hiyo kwa vipindi vitatu tofauti. 
Pia amechezea Tenerife ya Hispania na Lanus ya nyumbani kwao, Barcelona SC ya Ecuador na O'Higgins ya Chile.
Kabla ya kuwa kocha wa Newell, Martino aliifundisha kwa miaka minne Paraguay, kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.
Aliiongoza timu hiyo kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 matokeo mazuri zaidi kwa nchi hiyo daima kwenye mashindano hayo - kabla ya kufungwa 1-0 kwa mbinde na Hispania, walioibuka mabingwa.
At the helm: Martino managed the Paraguay to the World Cup quarter-finals in 2010
Martino aliifikisha Paraguay Robo Fainali Kombe la Dunia mwaka 2010
Watching: Barcelona players, including Carles Puyol, Messi and keeper Jose Manuel Pinto attended the announcement of Vilanova's resignation, given by president Sandro Rosell (below)
Wachezaji wa Barcelona, wakiwemo Carles Puyol, Messi na kipa Jose Manuel Pinto walihudhuria mkutano wa kujiuzulu kwa Vilanova ulioongozwa na Rais, Sandro Rosell (chini)
Rosell
Mwaka ulipfuata, Martino aliiwezesha Paraguay kutinga Fainali ya kwanza ya Copa America tangu mwaka 1979 ambako hata hivyo walifungwa 3-0 na Uruguay naye akajiuzulu mwezi mmoja baadaye.

MJUE GERARDO MARTINO

1962: Alizaliwa Novemba 20 mjini Rosario, Argentina.
1980-90: Kiungo huyo mshambuliaji anajiunga na Newell Old Boys ya Argentina na kuichezea mechi 392 za ligi, akifunga mabao 35 ndani ya miaka 10. Alitwaa taji la Primera Division mwaka 1988.
1991: Alicheza mwaka mmoja Tenerife na kuichezea mechi moja timu ya taifa yaArgentina chini ya Alfio Basile.
1991-94: Alirejea Newell Old Boys kwa miaka mitatu na kutwaa mataji mawili zaidi ya Argentina.
1994-95: Aliichezea kwa msimu mmoja Lanus kabla ya kurejea Newell Old Boys.
1996: Alikwenda Ecuadorian kuichezea mwaka mmoja Barcelona Sporting Club na kisha O'Higgins ya Chile.
1998: Alifanya kazi ya ukocha kwa mara ya kwanza Brown de Arrecifes.
1999: Alijiunga na Platense kama kocha.
2000: Alikuwa kocha Mkuu wa Instituto.
2002-03: Aliiongoza Libertad kutwaa mataji mawili ya Paraguay.
2004: Alitwaa taji la Paraguay akiwa na Cerro Porteno.
2005: Alikuwa kocha wa Colon kwa msimu.
2005-06: Alirejea Libertad na kutwaa taji la nne la Paraguay mwaka 2006.
2007: Februari - alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Paraguay na akashinda tuzo ya Kocha bora wa Mwaka Amerika Kusini.
2010: Juni - Aliiongoza Paraguay katika Kombe la Dunia Afrika Kusini na kuifikisha hadi Robo Fainali, ambako ilifungwa na Hispania.
2011: Baada ya Paraguay kufungwa katika Fainali ya Copa America na Uruguay, ajajiuzulu ukocha wa timu hiyo ya taifa.
2012-13: Alirejea Newell Old Boys kama kocha na kutwaa taji la Clausura mwaka 2013.
2013: Julai 23 - Anakubali Mkataba wa miaka miwili Barcelona, kurithi mikoba ya Tito Vilanova.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC