Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AZAM TV YAJITWISHA LIGI KUU

KAMATI ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana ilisaini makubaliano ya kuuza haki za kuonesha mechi za Ligi Kuu kwa Kampuni ya Azam Media Ltd kupitia kituo cha televisheni cha Azam Tv kwa kipindi cha misimu mitatu, kuanzia msimu huu wa 2013/14.


Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa TFF, Ilala jijini Dar es Salaam, Azam Media itamwaga kitita cha shilingi bilioni 5.560 ikiwa ni thamani ya mkataba huo ambao utasainiwa ndani ya siku 30 kuanzia jana.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia (Pichani), alisema kulikuwa na ofa nyingi za zabuni ya kuonesha mechi za Ligi Kuu (zikiwamo kutoka nje), lakini ofa ya Azam ni nono zaidi ambao watatoa asilimia 25 kabla ya kuanza kwa ligi hiyo Agosti 24.

Wallace alitumia fursa hiyo kuishukuru Azam kukubali kununua haki hiyo kwa ofa nono iliyozipiku kampuni kadhaa zikiwamo kongwe za kimataifa na kwamba wanajivunia kufanya kazi na kampuni ya kizawa iliyojitoa katika uwekezaji katika soka.

Akinuzngumza kwa niaba ya Rais wa TFF, Makamu wa Pili wa Rais Athumani Nyamlan aliwapongeza Azam Media Ltd kushinda manunuzi ya haki za kuonesha mechi za ligi kupitia kituo cha televisheni cha Azam Tv.

“Udhamini huu wa Azam Media Ltd, unastahili kupongezwa, hasa ukizingatia unakuja kipindi ambacho Tanzania kama taifa limeshaanza kunufaishwa na uwekezaji wa Kampuni SSB, ikiwamo kupitia michuano ya vijana ya Uhai Cup,” alisema Nyamlani.

Aliongeza Azam imefanya mengi ya kuigwa katika soka la Tanzania, lakini mkataba huu wa kwanza kwa kampuni ya nyumbani, unathibitisha utayari wa SSB katika kusaidia harakati za kuinua kiwango cha maendeleo ya soka nchini.

Akizungumza baada ya kutiliana saini kwa makubaliano hayo, Meneja wa Azam Media, Mzee Said Mohamed, alisema wamejipanga kufanya vitu vikubwa kupitia makubaliano hayo na kwamba kila Mtanzania atafurahia matangazo bora kupitia Azam Tv itakayozinduliwa Agosti 1.

Alibainisha kuwa, uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 30 wa kuanzishwa kwa Azam Tv chini ya Azam Media, unawapa uhakika wa matangazo bora ya televisheni ili kushinda vita ya pili ambayo ni ya ubora wa huduma zake kwa wateja hususani wapenzi wa soka.

“Nia ya makubaliano haya na mkataba baina ya Azam Media na Kamati ya Ligi wa haki za kuonesha mechi za Ligi Kuu, ni kunyanyua maendeleo ya soka letu kwa mchezaji mmoja mmoja, klabu na hatimaye taifa kwa ujumla,” alisema Mzee Said.

Alisema kuwa, Azam Tv itahakikisha katika msimu huu wa kwanza, angalau kila klabu inaoneshwa mechi zake mara nne na kwamba kituo hicho kitarusha moja kwa moja (live) jumla ya mechi 60, huku zingine 82 zikioneshwa baada ya kurekodiwa (Recorded).

Aliongeza kuwa, licha ya msimu huu kutarajia kutoa shilingi milioni 25 za maandalizi kwa kila klabu shiriki kama makubaliano hayo yanavyowaongoza, matarajio yao ni kuwa baada ya kumalizika kwa mkataba wa sasa, kila klabu kupata milioni 100 za maandalizi.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Azam Media Ltd inamiliki haki ya kufanya maelewano na kituo chochote cha televisheni ndani na nje ya nchi, ili kuweza kuonesha ‘live’ au marudio ya mechi za ligi kuanzia msimu huu wa 2013/14 unaoanza Agosti 24.

Mzee Saidi alibainisha kuwa, Azam Media Ltd itatoa asilimia 25 ya thamani ya mkataba kabla ya kuanza msimu huu, huku akifichua kuwa wamefurahishwa kushinda zabuni ya haki ya kuonesha Ligi Kuu na kuzipiku kampuni kubwa ambazo hata hivyo hazikutajwa.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo, kumefuatia mazungumzo kati ya Kamati ya Ligi na viongozi wa klabu za Ligi Kuu, ambapo mkataba huo utazipunguzia mzigo klabu ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ukata kwa kutegemea udhamini wa Vodacom peke yake, ambao hautoshi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC