ANCELOTTI AKWEPA MJADALA WA MAKIPA

Carlo Ancelotti 

Mkufunzi mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti alisema Jumamosi kuwa hataingizwa kwenye mjadala kuhusu nani kipa wake nambari moja, na kusema ana furaha kuwa na kipa mkongwe wa Uhispania Iker Casillas na Diego Lopez "makipa wawili wazuri."
"Sijui. La muhimu zaidi ni kwamba tuna makipa wawili wazuri na wenye uzoefu mwingi na stadi sana.
Tunahitaji makipa wawili wazuri kwa misimu yenye shughuli nyingi kama huu,” alisema Mwitaliano huyo.
Ancelotti amechukua tu hatamu kutoka kwa Jose Mourinho, ambaye alimweka benchi Nambari 1 ambaye hakuwa na mshindani Casillas, 32, msimu uliopita baada yake kurejea baada ya kupona jeraha la mkono, na alimpendelea Lopez.
Ancelotti alifichua kuwa Lopez ndiye atakayelinda wavu wakati wa mechi ya kirafiki ya Jumamosi dhidi ya klabu yake ya awali Paris Saint-Germain.