Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA YAIPIGA MWELEKA SIMBA, KUJENGA UWANJA WA KISASA BUNJU

Upo uwezekano mkubwa uwanja wa kisasa wa klabu ya Yanga ukajengwa mahali tofauti na Kaunda kutokana na udogo wa eneo la Jangwani, imeelezwa.

Akizungumza jana, mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini kwa sababu si msemaji wa masuala ya uwanja alisema:
Kwa kuangalia michoro ya uwanja mpya na mahali ambapo klabu inakusudia kujenga uwanja huo, ni vigumu uwanja ukawa kwenye eneo la Kaunda.
Alisema kutokana na kuwapo kwa ugumu huo, uongozi unaendelea kuangalia cha kufanya ili kufanikisha ujenzi huo, ambao umekuwa ukiahidiwa na awamu mbalimbali za utawala wa Yanga kwa miaka 20 sasa.
Mahasimu wa Yanga kwenye ligi kuu ya Bara, Simba, wanadai kuwa katika mchakato wa kujenga uwanja wake wa kisasa katika kitongoji cha Bunju, km 40 kutoka klabuni Msimbazi.
Uwanja wa Kaunda ulijengwa na waasisi wa klabu hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1970 lakini kwa sasa umezungukwa na makazi ya watu licha ya kuwa kwenye bonde la mto Msimbazi.
Ingawa uongozi wa Yanga ulikaririwa na gazeti moja mapema wiki hii ukidai umetuma maombi ya kunyakua nyumba hizo Wizara ya Ardhi, jambo hilo haliwezekani.
Kisheria mikono ya serikali imefungwa katika kutwaa makazi binafsi hayo kwa sababu uwanja huo si kwa ajili ya maslahi ya umma hivyo Yanga inatakiwa kushawishi majirani zake hao kuuza maeneo yao hayo kwake.
"Ukitazama michoro ni wazi pale hapatoshi lakini bado tunatafutwa njia nyingine za kuona ujenzi huo unafanikiwaje," alisema mjumbe huyo.
Alipoulizwa kama wanaweza kutafuta eneo lingine kwa ajili ya ujenzi huo, mjumbe huyo alisema hana uhakika lakini ikibidi watafanya hivyo.
"Nafikiri ukimtafuta makamu mwenyekiti (Clement Sanga) anaweza akakufafanulia kwa undani zaidi... mimi si msemaji.
"Lakini kikubwa ni klabu kuwa na uwanja wake hivyo kama pale patashindikana nafikiri kutakuwa na busara ya kutafuta eneo lingine."
Simu ya mkononi ya Sanga haikuwa ikipatikana alipotafutwa jana, hata hivyo.
Yanga imekabidhiwa michoro ya uwanja wenye kuketisha watazamaji 30,000 inaokusudia kujenga na mkandarasi kampuni ya Beijing Construction ambayo moja ya kazi zake nchini ni Uwanja wa Taifa wenye kuingiza watazamani chini kidogo ya 60,000.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC