Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA KUKIPIGA NA RAYON SPORT JIJINI MWANZA JULAI 6

MABINGWA wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC ya Dar es Saalaam watacheza na Rayon Sport ya Rwanda Julai 6 na 7, mwaka huu katika sehemu ya ziara yake ya kulitembeza Kombe lake la ubingwa wa Ligi Kuu mikoa ya kanda ya Ziwa, ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
TBL imekuwa ikiidhamini Yanga SC kupitia bia yake, Kilimanjaro Premeum Lager tangu mwaka 2008 sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba SC na ndiyo wamedhamini ziara hiyo.
Yanga SC itaondoka Dar es Salaam Julai 5, siku mbili tu baada ya kuanza  mazoezi Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Afrika Mashariki na Kati, Uwanja wa CCM Kirumba, Julai 6.
Na Julai 7, timu hizo ambazo zimewahi kufundishwa na kocha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Raoul Jean Pierre Shungu kwa wakati tofauti na kwa mafanikio, zitarudiana kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Baada ya hapo, mabingwa hao mara tano wa Kombe la Kagame (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati), Yanga SC wataelekea mjini Tabora, kucheza mechi nyingine na wenyeji, Rhino FC waliopanda Ligi Kuu msimu huu Julai 11, mwaka huu Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
Katika ziara hizo, Yanga watatembeza Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu, walilolitwaa kwa mara ya 24 msimu huu kwenye mitaa mbalimbali kushangilia na mashabiki wao. 
Yanga SC imeshindwa kwenda Sudan kutetea Kombe lake la Kagame mwaka huu, kutokana hofu ya machafuko yanayoendelea nchini humo na hii inakuwa mara ya pili kihistoria klabu hiyo kugoma kwenda kutetea taji hilo, baada ya awali mwaka 2000 kukataa kwenda Rwanda, hadi walipwe fedha zao za zawadi kwa kutwaa taji la mwaka uliotangulia 1999 mjini Kampala, Uganda.
Yanga SC, imekuwa na mafanikio makubwa tangu ianze kudhaminiwa na TBL, ikitwaa jumla ya mataji sita katika kipindi hicho, yakiwemo mawili ya Kagame, 2011 na 2012 na manne ya Ligi Kuu Bara, 2008, 2009, 2011 na 2013.
Katika kipindi hicho, hadhi ya klabu ya Yanga imepanda kutoka klabu isiyo na gari hata moja, hadi sasa kuwa mabasi matatu ya viwango tofauti, dogo aina ya Hiece, kubwa aina ya Coaster na kubwa zaidi aina ya Yutong kwa ajili ya safari za nje ya Jiji, ambayo yote wamepewa na wadhamini wao hao wakuu.
Kwa ujumla udhamini wa TBL umeleta ahueni kubwa ndani ya Yanga katika suala la uendeshaji wa timu, kutoka kwenye kushindwa kulipa mishahara ya makocha na wachezaji, hadi sasa kuwa na uhakika wa kufanya yote hayo sambamba na kusajili wachezaji ‘babu kubwa’ barani, kama Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda. Mkataba wa awali baina ya Yanga na TBL, ulisainiwa Agosti 18, mwaka 2008 katika hoteli ya Movenpick, mjini Dar es Salaam, ukiwa na thamani ya Sh bilioni 3 za Kitanzania na kwa miaka mitatu, ikiwa kila mwaka inapata Sh Bilioni 1, kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa timu 
Agosti 2, mwaka 2011, TBL ilisaini Mkataba wa udhamini na Yanga wa miaka minne sawa na kwa watani wao pia, Simba SC.
Katika mkataba huo mpya, uliotiwa saini kwenye hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam, TBL iliongeza dau la fedha za mishahara kwa wachezaji kutoka Sh. Milioni 16 hadi Milioni 25 kwa mwezi, ikaongeza basi moja kubwa, Yutong lenye uwezo wa kubeba abiria 54 na fedha kwa ajili ya kugharamia mikutano ya wanachama ya kila mwaka Sh. Milioni 20 kugharamia tamasha la mwaka la klabu na vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35 kila msimu.
Yanga pia inapewa bonasi ya Sh. Milioni 25 ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara au Milioni 15, ikishika nafasi ya pili katika Mkataba huo wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 5 tangu Agosti 8, mwaka huu hadi Julai 31, mwaka 2016.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC