
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akipokea vifaa mbalimbali vya michezo
kwa timu za baraza soka na netoboli kutoka kwa Meneja Masoko wa Kinywaji
cha Grandmalt, Fimbo Mohamed Butallah, wakati wa makabidhiano
yaliyofanyika kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar. Kushoto
ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi, mheshimiwa Hamza Hassan
Juma. Picha kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited
Timu za Baraza la Wawakilishi za mchezo wa soka na
netiboli, mwishoni mwa wiki zilikabidhiwa vifaa vya michezo vya aina
mbalimbali ili kuziwezesha kushiriki mashindano mbalimbali kwa uwezo
zaidi.
Vifaa hivyo vilitolewa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Idd, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo
Butallah alisema, wataendelea kuwekeza katika michezo kwani wanaamini
itatoa fursa kubwa kwa watu mbalimbali kushiriki na hata kujiongeza
vipato vyao.