Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wachezaji wetu mahiri kufurahisha jukwaa, Stars ndoto kupata ushindi wa uhakika

KARIBUNI wapenzi wasomaji kupitia Mtandao huu ambao kila siku ya jumamosi nimekuwa nikiwapatia makala mbalimbali za michezo hasa soka, Leo hii nimeamua kuwakumbusha kitu ambacho Watanzania wenzangu mlikuwa hamkifahamu.

Wasomaji wengi walinipigia simu wakinuunga mkono na kukubaliana na niliyoyasema, Wiki hii nawapa makala nyingine hususani kwa wachezaji wetu wa Kitanzania ambao wamekuwa wakisifika mbele ya mashabiki.

Kpoteza mwelekeo kwa timu yetu ya taifa, Taifa Stars na kupelekea kutolewa kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu fainali za kombe la dunia ambazo zitafanyika mwakani nchini Brazil.

Stars iliondoshwa na Ivory Coast baada ya kufungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani mabao 4-2, Matumaini kibao yalikuwepo kabla ya mchezo huo huku Watanzania tukijinasibu kuibuka na ushindi dhidi ya tembo hao wa Ivory Coast.

Kwa utashi wangu mapema kabisa kabla timu hizo hazijashuka uwanjani niliandika kupitia ukurasa huu kuwa Stars haitaweza kwenda Brazil na ni ndoto kubwa, Niliweka sababu kadhaa kuhusu kushindwa kwetu.

Na kweli matokeo yalitokea hivyo hivyo na kujikuta tunashindwa kufuzu kwenda Brazil huku tukiendelea kubaki kuwa watazamaji, Kikubwa kilichopelekea timu yetu kushindwa kwenda Brazil ni uwezo wetu mdogo hasa kwa wachezaji mpaka wasimaizi wakubwa wa mpira wa miguu nchini TFF na serikali kwa ujumla.

Mtanzania kila unayemuona ni kocha, Mchambuzi, Na hajulikani nani mchezaji au kiongozi huku kila mmoja ni bingwa wa kushusha visingizio kwa mwenzake, Lakini ukweli wa yote bado sana Watanzania kufikia maendeleo yanayotakiwa.

Tatizo la Watanzania tunapenda sana kushirikisha siasa kwenye soka au michezo mingineyo, Hata tasnia ya urembo imeingiliwa  na siasa na ndio maana Tanzania inashindwa kupata mafanikio katika nyanja za kimataifa.

Mchezo wa soka umeingiliwa tena sana na umegeuzwa kichaka cha wanasiasa, Tazama michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati inaendelea vema nchini Sudan katika mji wa Darfur ambapo siasa za Watanzania zimeziponza timu zote za Simba na Yanga ambazo zilikuwa wawakilishi pekee.

Tuachane ni hilo na sasa tuingie kwenye mada husika, Wachezaji wa TAanzania nao ni tatizo tena kubwa kwa maendeleo ya soka la nchi hii, Wachezaji wetu hasa wale waliopo kwenye timu ya taifa wanashindwa kumuelewa kocha wao Kim Poulsen na wanachokifanya wengi hamjakielewa.

Kikosi cha timu ya taifa kilichoundwa na mchanganyiko wa wachezaji kutoka vilabu kadhaa hapa nchini hawachezi kitimu na kuweza kuleta mafanikio, Lakini Watanzania bado wanajidanganya kuwa Stars ilicheza vizuri tulipocheza na Ivory Coast na tatizo lilikuwa moja tu yaani kukosa bahati.

Wenzetu Ivory Coast walizitumia nafasi zao vizuri lakini sisi tulishindwa kuzitumia nafasi vizuri na kupelekea kipigo hicho, Wngine wanajidanganya kuwa tulikosa uzoefu huku wenzetu walitumia uzoefu wao wa kucheza mechi nyingi za kimataifa pamoja na kujaza wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Haya yote mimi sikubaliana nayo, Tatizo la wachezaji wa Tanzania si muda mfupi ila ni la muda mrefu huenda kabla hajafika Marcio Maximo ambaye ndiye aliyekuja kulibadili soka la nchi hii.

Kim Poulsen amekuja kuendeleza ya Maximo na si kuleta soka jipya kama watu wanavyojidanganya wakati tulipotoka kucheza na Morocco pamoja na Ivory Coast, Wachezaji wa Tanzania wamezoea kucheza na jukwaa.

Na imekuwa kawaida yao kwa kipindi kirefu huku akili za mashabiki wa Tanzania zikiwa nyuma yao, Mpira hauchezwi kwa kufurahisha jukwaa kama ilivyo kwa wachezaji wa Tanzania na ndio maana tulikubali haraka kipigo cha Ivory Coast.

Kama wachezaji wetu wakicheza kwa lengo la kushindana na Ivory Coast huku wakiacha ule mchezo wao wa kutaka washangiliwe jukwaani na kuweka mikakati ya kutafuta magoli nina imani ushindi ungepatikana, Tanzania tunao wachezaji wazuri wanaoonyesha soka maridhawa lakini uwezo wao ni jukwaa tu na sivinginevyo.

Hakuna mikakati iliyo makini kuhakikisha tunapata ushindi, Kwa mfano sikuona umuhimu wa Mwinyi Kazimoto, Ni mchezaji mzuri lakini anacheza na jukwaa, Hakuna la maana alilokuwa akilifanya uwanjani na ndio maana hata 'maproo' wa Ivory Coast hawakuridhishwa naye.

Salum Abubakar 'Sureboy' ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora anayechipukia na chama cha wachezaji Sputanza, Kiwango chake ni kizuri lakini anacheza na jukwaa, Na kama Kim Poulsen ataendelea kuwang' ang' ania wachezaji wa namna hii basi Stars haitafika kokote.

Wachezaji wapo wengi tena wanacheza soka la kuvutia kuliko hata hao waliopo Stars tatizo lililopo ni kung'ang'ania damu ile ile, Hawataki kubadilika kila kukicha ni walewale na ndio maana nafasi yetu kimataifa inabaki pale pale.

Nikiwa na jamaa yangu mmoja anitwaye Mohd Nteze yeye aliwahi kunisimulia juu ya thamani ya timu yetu ya taifa, Taifa Stars kuwa miaka nenda rudi nafasi yake katika mashindano yoyote ni ya tatu na ikijitahidi imefungwa kwa taabu.

Maneno ya rafiki yangu yule nimeona yana ukweli ndani yake na kuanzia sasa nimekubaliana naye moja kwa moja, Nafasi ya Tanzania ni ya tatu na hilo limejidhihirisha, Wachezaji wa Stars wanaona ufahari kushangiliwa jukwaani kwa kandanda lao zuri pasipo kutafuta magoli.

Wapo wanaojituma na wanastahili kucheza Stars lakini hao niliowataja ilistahili kubadilika, Waache kucheza na jukwaa na waangalie kazi yao iliyowatuma, Tnajua mpira lazima upate sapota kutoka kwa mashabiki lakini soka lao linaishia kupiga chenga nyingi na kupiga darizi muda wote huku wakisahau muda unakwenda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC