Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TUZO KAMA HIZI ZINAPOTOSHA UKWELI

MWISHONI mwa wiki iliyopita kulikuwa na tukio la kushangaza tena la kufurahisha kwa wadau wa michezo hususani soka, Chama cha wanasoka nchini  SPUTANZA kiliamua kutoa tuzo zake kwa wachezaji waliofanya vizuri katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom ya msimu uliomalizika wa 2012/13
.

Cha kushangaza hadi kunifanya niandike makala yenye kushangazwa na utoaji wa tuzo hizo ni sehemu chache nyingine zote wamepatia, Kwanza ningeanza
Wamefanya kitu kizuri sana na kinachohitaji pongezi, Si kwa kuzingatia wajibu wao kama wapenda michezo hasa soka, Ni kutokana na mawazo yao yaliyopelekea kuybuni kitu kizuri kwa kutengeneza tuzo hizo kwa wanamichezo.

Sputanza nawapongeza kwa kukaa na kufikiria na kuanzisha tuzo hizo, Wengi watashangazwa na ujio wao mwaka huu na kushangaa walikuwepo wapi miaka yote hiyo!, Lakini kila siku maendeleo huongezeka.

Lakini nashangazwa na jinsi ya kuwazawadia wanamichezo bora pasipo kuzingatia vigezo husika, Kwa mfano kama wangekaa chini ya kutoa tuzo hizo kwa wahusika ingekuwa bonge la mapinduzi katika utoaji wao tuzo mwaka huu.

Lakini wamekosea kutoa tuzo hizo, Tuanze na tukio zima la utoaji tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa 2012/13 ambayo ilimalizika hivi karibuni huku Yanga ikifanikiwa kutwaa ubingwa, Azam FC ilifanikiwa kukamata nafasi ya pili, Simba ilishika nafasi ya tatu na Kagera Sugar iliambulia nafasi ya nne.

Sputanza imeshindwa kuzingatia vigezo na kukurupuka kutoa tuzo ambazo zinaweza kushangaza zaidi ninavyoshangaa mimi, Katika kamati yake ya uandaaji tuzo hizo haikujumlisha wanamichezo wenye weledi wenye kujua mbivu na mbichi.

Wametangaza tu tuzo zao na kutushangaza sisi tunaojua nini maana ya tuzo, Siku zote tuzo hupewa anayestahili na asiyestahili hawezi kupewa tuzo, Sputanza wallitangaza kuwapa tuzo za kufanya vizuri kwa wanamichezo mbalimbali wanaotokana na ligi kuu.

Tuzo ya kocha bora ilikwenda kwa Meck Mexime wa Mtibwa Sugar nadhani kwa kuiwezesha timu yake kukamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara, Pia kipa bora alichukua Hussein Shariff 'Cassilas' pia wa Mtibwa.

Wakati tuzo ya kipa bora ikienda kwa Cassilas wa Mtibwa, Mchezaji bora wa mwaka Amri Kiemba, Na mchezaji bora anayechipukia ilikwenda kwa Salum Abubakar 'Sureboy' wa Azam, Hapo ndipo ninaposhangazwa na utoaji wa tuzo hizo kwa kutozingatia vigezo na masharti, Anapewaje kocha bora Meck Mexime wakati hajaweza kuifikisha timu yake ya Mtibwa kwenye tatu bora.

Wamezingatia vigezo gani au kuna upigwaji wa kura ulitumika, Tuzo hizo zilizokjuwa zikidhaminiwa na kampuni ya Pepsi inayodhalisha vinywaji baridi aina ya soda za Pepsi, Mirinda na 7up.

Tuzo hizo zilijulikana  kwa jina la Spuntanza Pepsi Award,  Nilidhani tuzo hizo zinatolewa kwa mara ya kwanza kwa kufuata vigezo, Kumbe Sputanza wamekuja kuvuruga kabisa mwenendo mzima wa maendeleo ya michezo hapa nchini.

Miaka mingi Sputanza wamekuwa katika malalamiko mengi kuhusu mwenendo mzima wa soka huku wakidai kusahaulika na wadau wa soka, Kumbe hawako sahihi katika muendelezo mzima wa soka la nchi hii na wanachokifanya wadau kukipuuzia ni sawa kabisa. 

Mexime hakustahili kuwa kocha bora mbele ya Ernie Brandts wa Yanga, Stewart Hall wa Azam au Abdallah Kibaden wa Kagera Sugar, Pia bado hajaweza kumshawishi mtu kumpa tuzo hiyo mbele ya Patrick Liewig aliyeifikia kati ligi kuu ya bara.

Inashangaza sana Mexime anapewa heshima hiyo wakati timu yake ilipokea kipigo kikubwa cha mabao 4-0 mbele ya Azam inayonolewa na Hall, Pia timu yake ya Mtibwa ilikamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi wakati Kibaden wa Kagera aliingia kwenye nne bora.

Hata kama waliangalia wazawa na ndio maana wakamnyima tuzo raia wa Ivory Coast Kipre Tchetche wa Azam, Lakini Mexime bado hajaweza kumshawishi mdau wa soka kumpa tuzo ya kocha bora mbele ya Kibaden, Moroco wa Coastal Union ambaye aliiwezesha timu yake kukamata nafasi ya tano.

Nashangaa zaidi na zaidi Hussein Shariff 'Cassilas' wa Mtibwa anapewa tuzo ya kipa bora wakati hayupo kwenye timu ya taifa na wala timu yake haikuwepo tatu bora, Unapotaja makipa bora nchi hii ni Juma Kaseja, Mwadini Ally na Ally Mustapha 'Barthez'.

Shariff alistahili kupewa tuzo ya kipa anayechipukia na si kipa bora, Sputanza wamechemka tena sana na wanachotakiwa ni kuwaomba radhi Watanzania kwa tuzo zao za uongo, Tuzo hizo zinachangia kuwaharibia mipango wachezaji waliofanya vizuri msimu uliopita na kuwasafisha wale wenye viwango vidogo.

Naona kama Sputanza iliamua kuwaridhisha tu hao akina Mexime na Cassilas kwa malengo yao binafsi lakini si kwa kiwango, Bado sana Mexime kuwavuka makocha hao niliowataja ambao wameleta mapinduzi makubwa katika soka msimu uliopita.

Mtibwa aina cha kujivunia zaidi ya kuzikamia Yanga na Simba peke yake, Na hakuna ilichofanuya katika mchezo huo wa soka hususani katika ligi iliyomalizika, Azam ambao walifika hatua ya 16 bora kombe la shirikisho barani Afrika chini ya kipa wake Mwadini Ally alistahili kupata tuzo hiyo.

Juma Kaseja ambaye ndiye nambari moja katika timu ya taifa huwezi kumfananisha na Cassilas ambaye hakufanya lolote la kushangaza msimu uliopita, Ndio maana nikasema labda angepewa tuzo ya kipa bora anayechipukia kwa maana hawezi kuwazidi Barthez, Kaseja na Mwadini.

Amri Kiemba nakubaliana nao kwa sababu hakuna atakayepinga kiwango chake msimu uliomalizika wa ligi pamoja na sasa kwenye timu ya taifa, Kiemba nampa asilimia mia moja kuwa mchezaji bora kila tuzo itakayoandaliwa lakini siyo hii ya uongo iliyotolewa na Sputanza.

Sikubaliana nayo kwa kuwaongopea Watanzania kuwa Meck Mexime kocha bora huo ni uongo tena usiotakiwa, Sina ugomvi wowote na watu hao wala sijawahi kukorofishana nao lakini nazipinga tuzo hizo kwa nguvu zote

kuwapongeza waandaaji wa tuzo hizo Sputanza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC