Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TANZANIA KUMWAGIWA NEEMA NA OBAMA

Rais Jakaya KIkwete akisalimiana na Rais wa Marekani, Barack Obama katika Ikulu ya White House nchini Marekani. Akiwa nchini Rais Obama atafanya mazungumzo na Kikwete kisha watafanya mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari.

Ukitaka kumfahamu mtu, tazama aina ya watu wanaomzunguka. Msemo huu unaweza kutumika kuielezea Tanzania hasa baada ya kupata fursa ya kutembelewa na marais watatu wa taifa lenye nguvu zaidi duniani, Marekani.
Kwa mara ya kwanza, Tanzania ilitembelewa na Rais wa Marekani aliyeko madarakani, George W Bush mwanzoni mwa 2008 na sasa nchi imepata fursa tena ya kutembelewa na rais mwingine wa nchi hiyo, Barack Obama ambaye atakuwa ameambatana tena na Bush, jambo ambalo ni la kihistoria katika Bara la Afrika.
Pamoja na kwamba kuna hali ya kutoridhika na hali halisi ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya Watanzania, hali inaonekana kuwa ni tofauti kabisa kwa Marekani ambayo mtazamo wake wa masuala ya nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa mengi ya magharibi.
Akizungumzia sababu za ziara hiyo kwa njia ya conference call kutoka Washington, Naibu Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ikulu ya Marekani, Gayle Smith alisema Obama anazuru Tanzania kwa sababu nchi hiyo ni rafiki mkuu wa Marekani katika Afrika Mashariki na kwamba imebobea katika misingi ya kidemokrasia.
Smith alisema Bara la Afrika hususan Tanzania ni moja ya masoko muhimu sana yanayoibukia ulimwenguni na Marekani ni lazima iongeze harakati zake barani humo.
“Kuna fursa nyingi za kiuchumi, biashara na uwekezaji jambo ambalo linaitisha umuhimu wa kampuni na biashara za Marekani kujikita zaidi Afrika,” anasema Smith.
Tofauti na ziara ya Bush ambayo ililenga zaidi kuisaidia Tanzania kutoa huduma bora kwa watu wake hususan afya; ziara ya Obama imetokana na maombi na msukumo kutoka kwa wafanyabiashara wa Marekani ambao waliitaka Serikali yao kuunda mikakati ya makusudi ya kuhakikisha nchi hiyo inakuza na kuboresha uhusiano wa kibiashara na Waafrika.
Wakati wa ziara ya George W Bush, Tanzania ilinufaika na msaada wa dola 698 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vyandarua na dawa za kuulia mbu pamoja na kuendeleza mapambano dhidi ya Ukimwi.
Maambukizi ya Ukimwi yalianza kushuka mwaka 2008 kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi kufikia asilimia tano na mwaka huu.
Idadi ya watu ambao wanajitokeza kupimwa Ukimwi na kuchukua majibu yao imeongezeka kutoka asilimia 20 ya wanawake mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 30 mwaka 2012 na kwa wanaume imepanda kutoka asilimia 19 mwaka huohuo na kufikia asilimia 27 mwaka 2012.
Kwa upande wa malaria, kaya tisa kati ya 10 zinatumia vyandarua vyenye dawa ongezeko ambalo ni mara nne zaidi ya idadi ya kaya zilizotumia vyandarua hivyo mwaka 2004.
Hali kadhalika, zaidi ya asilimia 70 ya watoto ambao wako hatarini kuambukizwa malaria walilala ndani ya vyandarua ongezeko ambalo pia ni mara nne zaidi ya idadi ya mwaka 2004.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC