UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba jana umetangaza rasmi kuachana na kipa wake namba moja Juma Kaseja baada ya kumalizika mkataba wake, Akizungumza jana mwenyekiti wa kamati ya usajili Zackaria Hanspope amedai kuwa klabu ya Simba haina mpango wa kumuongeza mkataba kipa huyo.
Amedai kuwa Kaseja alikuwa akihitaji dau kubwa la fedha tofauti na wao walivyopanga kumpa, Kaseja alikuwa akitaka kulipwa milioni 40 wakati Simba ilitenga milioni 20 ili kumsainisha tena, Taarifa zilizotufikia Mambo Uwanjani zinasema kuwa Simba haikutaka kumpa fedha hizo kutokana na huduma ndogo ya kipa huyo mkongwe.
Kaseja hawezi kulipwa kiasi hicho cha fedha kwakuwa umri wake ni mkubwa hivyo hawezi kuitumikia Simba kwa muda mrefu, Simba sasa inasuka upya kikosi chake na imekuwa ikisajili vijana, Tayari klabu hiyo inao makipa watatu ambao ni pamoja na Abbel Dhaira, Andrew Ntala na Abuu Hashim.
Hanspope aliwataka mashabiki wa Simba kutulia na kuwaachia wao viongozi ili kufanya usajili makini utakaokuwa na faida kubwa na klabu hiyo kwa siku zijazo