
Sino ni mshambuliaji amesajiliwa na Simba akitokea
Prisons ya Mbeya kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo mshambuliaji
Malceli na beki wa kushoto Omary wamepandishwa kutoka Simba B.
mtanda huu uliwashuhudia wachezaji hao wakisaini
kwenye ofisi za Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Kinesi’
Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia usajili huo, Itang’are
alisema,”Katika kuhakikisha hatufanyi makosa tumemalizana na wachezaji
hawa kwa lengo la kuiboresha timu katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.”
Alisema,”Tumewasajili vijana hawa baada ya kufanya
majaribio na makocha wameridhika na viwango vyao kwa kipindi chote cha
majaribio,”alisema Itang’are.
Naye, Sino akizungumzia kusajiliwa na Simba
alisema amefurahishwa na benchi la ufundi la Simba kwa kumwamini na
kumjumuisha kikosini hapo, hivyo ameahidi kuifanyia kazi nzuri klabu
hiyo ya mtaa wa Msimbazi.
“Nashukuru kuchaguliwa Simba, nawaahidi mashabiki nitawafanyia kazi nzuri, kikubwa naomba ushirikiano wao,”alisema Sino.
Naye Malcel alisema,” Nimefurahi kusajiliwa Simba
na sasa najipanga kuhakikisha naifanyia mazuri klabu hii kwenye ligi na
mashindano mengine yatakayotukabiri.”
Kwa upande wa Omary yeye alisema atajitoa kwa nguvu zote kuifanya Simba ing’are.
Tayari Simba imempa mkataba tena Amri Kiemba,
imemsajili beki Samwel Senkoon raia wa Uganda kutoka URA, imemsajili
Andrew Ntala kutoka Kagera Sugar, Ibrahim Twaha ‘Messi’ kutoka Coastal
Union ya Tanga na wengine wa timu B kama Ramadhani Singano ‘Messi’,
Hassan Khatib na Edward Christopher.
Katika hatua nyingine, Simba iliifunga timu ya
Kiluvya bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa juzi kwenye Uwanja
wa Kinesi jijini Dar es Salaam.
Bao hilo la Simba lilifungwa na Sino kutokana na pasi ya Malcel.