Ruka hadi kwenye maudhui makuu

POULINHO AIPELEKA BRAZIL FAINALI KOMBE LA MABARA IKIIUA URUGUAY 2-1, FORLAN AKIKOSA PENALTI


Paulinho ameibeba Brazil

IBAO la kichwa la Paulinho zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho, limeipa Brazil ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay usiku wa kuamkia leo na kutinga Fainali ya Kombe la Mabara.
Diego Forlan alikosa penalti dakika ya 13, baada ya beki wa Chelsea, David Luiz kumuangusha Diego Lugano kwenye eneo la hatari.
Brazil ilipata bao la kuongoza dakika ya 40, wakati Neymar alipoitokea pasi ndefu ya Paulinho na kuingia ndani kisha kufumua shuti lililombabatiza beki wa Uruguay kabla ya kumkuta Fred, aliyefunga.
Iliwachukua Uruguay dakika tatu tangu kuanza kipindi cha pili kusawazisha bao hilo, baada ya mabeki wa Brazil kuzembea kuondosha mpira kwenye eneo la hatari wakati pasi hafifu ya Thiago Silva ilipomkuta Edinson Cavani aliyefunga.
Fainali ya michuano hiyo 'amsha amsha' kuelekea Fainali za Kombe la Dunia, itapigwa mjini Rio de Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana Jumapili.
Brazil ilibadilisha kikosi kutoka kile kilichoifunga Italia katika mechi yao ya mwisho ya Kundi A, ikimuanzisha Paulinho badala ya Hernanes katika kiungo.
Uruguay ilimuacha nje Abel Hernandez, mshambuliaji kinda wa Palermo, ambaye alifunga mabao manne dhidi ya Tahiti katikati ya wiki, na kuwaanzisha kwa pamoja mbele ya mdomo wa goli Luis Suarez, Diego Forlan, na Edinson Cavani.
Huo ni ushindi wa nne mfululizo kwa Brazil katika michuano ya mwaka huu na wao tano kwa jumla chini ya kocha Luiz Felipe Scolari, kasi ambayo inaweza kuwainua kutoka nafasi ya 22 katika viwango vya FIFA, nafasi ya chini zaidi kwao kuwahi kushika daima.
Pia unaendeleza rekodi ya kutofungwa na wapinzani wao hao wa Amerika Kusini katika mechi nane sasa tangu Julai 2001.
Katika mchezo huo, kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar/Hernanes dk72, Gustavo, Paulinho, Fred, Hulk/Bernard dk64 na Neymar/Dante dk90.
Uruguay: Muslera, Lugano, Godin, Caceres, Maxi Pereira, Rodriguez, Arevalo Rios, Gonzalez/Gargano dk83, Forlan, Suarez na Cavani.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC