Miss Tabata 2013, Dorice Mollel (22) yupo nchini
Ujerumani kwa ziara ya wiki tatu ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi
hiyo na Tanzania.
Dorice ambaye ni mwanafuzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Kumbumbumbu ya Mwalimu Nyerere ni mmoja ya wanafuzi 10 kutoka nchini waliochaguliwa kwenda mjini Hamburg na Berlin kudumisha ushirikano na kujifunza tamaduni za Kijerumani.

Mratibu wa Miss Tabata, Joseph Kapinga alisema jana jijini Dar es
Salaam kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na MitOst Hamburg ya Ujerumani na
Tanzania Youth Coalition.
“Tunashukuru sana hii ni nafasi pekee kwa Dorice kujifunza mambo
mengi kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Ilala ambalo limepangwa
kufanyika Agosti. Tuna imani ziara hii itapanua mawazo yake na atakuwa
tishio kwenye shindano hilo la urembo,” alisema Kapinga.
Dorice ambaye alishinda taji la Miss Tabata Mei 31, aliondoka nchini Juni 6 na atarejea Julai 5.