
Timu zote, Norwich na Swansea ziko tayari kulipa Pauni Milioni 6 kuununua Mkataba wa mchezaji huyo.
Lakini nyota huyo wa Ivory Coast anataka
kuungana na kocha wake wa zamani, Roberto Martinez, ambaye amehamia
Goodison Park mwezi uliopita.
Alikuwa Martinez aliyemvuta Kone, mwenye umri wa miaka 29, England miezi 12 iliyopita kwa Pauni Milioni 3.5 kutoka Levante.
Na mshambuliaji huyo anaamini Mspanyola huyo anaweza kumfanya aendelee kuwa bora katika Ligi Kuu ya England.