![]() |
|
|
|
Beki wa kushoto wa klabu ya Simba SC na timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars Shomari Kapombe yupo majaribioni na klabu ya FC
Twente inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Uholanzi Eredivisie, baada ya
klabu hiyo kutangaza rasmi kwenye tovuti yao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alieanzia kuchezea mpira timu ya Polisi Morogoro ambaye amekua kwenye fomu ya hali ya juu katika ngazi za klabu na timu ya taifa pia alituzwa tuzo ya mchezaji bora kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania msimu uliopita.
"Klabu yake ya Simba imempatia ruhusu kuja na kujaribu bahati yake nje. Wamempa mwangaza mkubwa kwenye majaribio yake huku ulaya, na kumtakia mafanikio makubwa," taarifa rasmi kwenye tovuti yao fctwente.nu ilisema.
Kapombe ambaye mkataba wake na Simba unaisha mwisho wa mwaka huu, atakuwa mchezaji wa pili wa kiafrika kwenye kikosi cha FC Twente pamoja na mchezaji wa Ghana Eghan Shadrach endapo ataweza kufaulu majaribio yake.