Kamati ya ligi yaichimba mkwara Yanga

KAMATI ya ligi jana imeweka hadharani kuwa endapo mabingwa wa soka nchini Yanga watashindwa kuudhuria sherehe za utoaji zawadi za washindi ligi kuu ya Vodacom itakiona chamoto, Mwenyekiti wa kamati Wallace Karia amesema kuwa haoni sababu za Yanga kugomea zawadi hizo.


Sherehe za kukabidhi zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitafanyika Julai 3 na mgeni rasmi ni waziri wa habari michezo na utamaduni Mhe Fenella Mukangara, Yanga imetangaza kususia sherehe hizo za utoaji wa zawadi kwa madai ya kucheleweshwa.

Kupitia msemaji wake Baraka Kizuguto, Yanga imetangaza kutoudhuria katika utoaji wa zawadi hizo kwa madai ya kucheleweshewa zawadi zao ikiwemo fedha za ubingwa, Sababu za Yanga zimepingwa vikali na kamati ya ligi ambapo yenyewe imesema hata Yanga isipoudhuria sherehe hizo zitafanyika.

Karia amesisitiza kuwa Yanga ni kitu gani hata kama wamesusia ni bora wasusie na zawadi zenyewe, Ameongeza kuwa hawataibembeleza kwa lolote kwani wanaostahili kupewa zawadi si wao peke yao.

Yanga imemaliza kama mabingwa wa bara wakati Azam ikishika nafasi ya pili huku Simba ikikamata nafasi ya tatu, Kagera Sugar ilishika nafasi ya nne ambapo pia zinastahili kupata zawadi zao, Kama Yanga ikikataa itawanyima nafasi wachezaji wake ambao wengine wanastahuili kupewa zawadi ya uchezaji bora au mchezaji mwenye nidhamu