KITUO cha Redio cha Napoli, Marte
kimetangaza kwamba dau la Pauni Milioni 49.3 limetolewa na Chelsea kwa
ajili ya mshambuliaji Edinson Cavani.
Katika taarifa ya jana usiku, Radio
Marte ilitangaza: "Tumepokea taarifa kutoka ofisini kwa vyanzo vya
kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili la kuiuzia Chelsea Cavani.
"Rafa Benitez pia amebariki, lakini
kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka kupata mshambuliaji atakayeziba
pengo la Il Matador.
"Aurelio De Laurentiis", klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
"Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,". Habari zimevuja kama kwamba Cavani
ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis
na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo.
Mshambuliaji huyo wa Uruguayna baba yake
awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real Madrid. Klabu hiyo ya
Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa itabidi waipiku ofa
iliyotolewa na Chelsea.

Anayetakiwa sana: Man United na PSG pia zinamtaka Cavani