Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wachezaji wageni Ligi Kuu kubanwa

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema litakutana na klabu za Ligi Kuu kuzikumbusha azimio la mwaka jana la mjini Bagamoyo kuhusu wachezaji wa kigeni.

Azimio hilo lilipitisha sheria inayokataza klabu za Ligi Kuu kusajili zaidi ya wachezaji watatu kutoka nje ya nchi.
Pamoja na sababu mbalimbali za kupitisha azimio hilo, dhamira kuu ilikuwa kuwapa fursa wachezaji wa ndani kuonyesha vipaji vyao kwenye michuano ya ligi.
Kwa sasa, klabu zinaruhusiwa kusajili siyo zaidi ya wachezaji watano kufikia msimu uliomalizika, lakini kama azimio hilo litaungwa mkono na klabu, basi msimu wa 2013/14 utashuhudia wachezaji wachache wa kigeni.
Klabu za Simba, Yanga na Azam ndizo zinaoongoza kusajili wachezaji wa kigeni kulinganisha na timu zingine zinazoshiriki ligi hiyo.
Mtendaji Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alikaririwa na mtandao wa soka nchini Uganda, akisema mchakato huo unaendelea kufanyiwa kazi na watakutana na viongozi wa klabu kujadili.
“Ni sheria mpya ya Azimio la Bagamoyo. Ni vyema sheria zilizowekwa na sisi wenyewe zikaheshimika. Tutakutana na klabu kujadili azimio hili,” alisema Osiah.
Kabla hata ya kufanyika kwa kikao hicho, klabu hizo zenye utamaduni wa kusajili wachezaji wa kigeni, zilionyesha kutoridhika nalo.
Katika msimu uliopita klabu ya Azam ilikuwa na wachezaji wa kimataifa kutoka Kenya, Joackins Atudo na Humphrey Mieno, Brian Umony kutoka Uganda na wachezaji wawili kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche na Michael Bolou.
Kwa upande wa Yanga, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Mganda Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wa Burundi na Mbuyu Twite, huku Simba ikiwa na Abel Dhaira, Musa Mudde, Felix Sunzu na Komabil Keita.
Pamoja na tahadhari hiyo, klabu hizo zimeendelea na zoezi la kusajili wachezaji wa kigeni bila kufikiria uwepo wa azimio la Bagamoyo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC