Jina lake halisi ni Albert Keneth Mangweha, ana asili ya Ruvuma
(Mngoni) lakini alizaliwa Mbeya 16 Novemba 1982 akiwa mtoto
wa mwisho. Kwa baba yake alikuwa mtoto wa 10 na kwa mama
ni mtoto wa 6 kuzaliwa.
Akiwa na miaka 5 alihama Mbeya na kuhamia Morogoro na kusoma
Shule ya Msingi Bungo hadi darasa la 5 na kisha kuhamia Dodoma
akiwa na Baba yake na kumalizia Shule ya Msingi Mlimwa.
Alisoma Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi Mazengo Mjini Dodoma.
|