
Na Prince Hoza
MDAU maarufu wa vipindi ya redio hapa jijini Beatrice Shadrack ama eatrie wa Kariakoo ukipenda Sister dread wa ukweli Mama Balotelli wa Tz (Pichani) amenusurika kufa asubuhi ya leo baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki.
Akizungumza na mtandao huu Peter Tosh ambaye naye ni mdau wa media amesema kuwa Mama Balotelli alipata ajali ya pikipiki katika maeneo ya Buguruni.
Inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa pikipiki ndio umechangia kutokea kwa ajali hiyo, Ingawa mpaka sasa mdau huyo maarufu katika vituo vya redio anaendelea vizuri baada ya kupata huduma ya kwanza ila ameumia mguu wake wa kulia