Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KIBADEN NOMA, AANZA KAZI SIMBA

Kocha Abdallah 'King' Kibadeni (mwenye miwani) akizungumza na wachezaji wapya wanaowania kusajiliwa Simba wakati alipoanza rasmi kazi ya kuifundisha timu hiyo katika mazoezi yao kwenye uwanja wa Kinesi, jijini Dar es Salaam jana.
 
Kocha Abdallah 'King' Kibadeni jana alianza rasmi kuifundisha Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Mfaransa Patrick Liewig aliyetupiwa virago.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, jana asubuhi aliongoza mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam, ambayo yalihudhuriwa na wachezaji 11 wapya, wakiwamo Wacongo wanne.

Kibadeni maarufu kama 'King Mputa' ametua Simba ikiwa ni mara yake ya nne, akitokea Kagera Sugar aliyoinoa msimu uliomalizika wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya nne na ya mwisho ya kufuzu kucheza michuano midogo ya Ligi ya Super8.

Mkongwe huyo aliiambia MAMBO UWANJANI  mazoezini hapo jana kuwa anafuraha kusaini mkataba huo na kwamba malengo yake ni kuhakikisha Simba inafika mbali katika ligi ya nyumbani na kimataifa kama ilivyo desturi yake.

Kibadeni aliyewahi kuifikisha Simba kwenye fainali ya michuano ya CAF mwaka 1993 ambapo walifungwa 2-0 dhidi ya Stella Abidjan, alisema kitu cha muhimu anachopenda ni kupewa muda ili afanye kazi zake.

"Nimetua rasmi Simba kwa mkataba wa miaka miwili na matarajio yangu ni kuifikisha mbali. Mashabiki watarajie lolote katika michuano ya Kagame kutokana na muda mfupi uliopo, lakini katika ligi wasiwe na shaka," alisema.

Aliongeza anachopenda kwa uongozi wake ni kupewa nafasi ya kufanya kazi bila kuingiliwa ili mwisho iwe rahisi kwao kumbana.

"Hakuna jambo ambalo silipendi kama kuingiliwa kazini, kila mtu atekeleze majukumu yake. Benchi la ufundi tuachwe tuifanye kazi na wataona nini tutakachokifanya kwani najiamini naweza," alisema Kibadeni.

Kuhusu wachezaji waliosimamishwa na uongozi kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, Kibadeni alisema hawana nafasi kwake kwa kuwa siku zote yeye amekuwa muumini wa suala la nidhamu kwa wachezaji.

"Kama viongozi waliwasimamisha kwa utovu wa nidhamu, kwangu pia hawana nafasi ili wasije wakaniharibia kazi, nitafanya kazi na wachezaji wote walio tayari kuitumikia Simba kwa hali na mali ili ifike mbali," alisema.

Makocha wasaidizi waliompokea Kibadeni, Jamhuri Kihwelu 'Julio', Seleman Matola na Amri Said walisema wamefurahia ujio wa mwalimu huyo aliyewahi kuwanoa enzi za uchezaji na kuamini benchi la ufundi sasa limekamilika na Simba itatisha.

"Simba ijayo itatisha, nani asiyemjue Super Coach King Kibadeni, hebu piga picha huku King, hapa Julio aaah Simba itatakata tuombe Mungu, ila tumefurahi mno kurejeshwa kwa Kibadeni Msimbazi," alisema Julio.

Katika hatua nyingine jumla ya wachezaji 11, wakiwamo watano kutoka nje ya nchi jana walijitokeza kwenye majaribio ya kuwania kusajiliwa Simba yaliyosimamiwa na makocha wa Simba akiwamo kocha mkuu Kibadeni.

Wachezaji hao kutoka DRC ni Fabian Tshayaz, Fabrice Balou na Patrick Milambo wote kutoka klabu ya AS Vita na Joe Fils kutoka Le Verez Club.

Wengine waliojitokeza kuomba kazi Msimbazi ni Mohammed Abdallah aliyekuwa anachezea Ferreviario De Nampula ya Msumbiji, Adeyun Saleh wa Miembeni Zanzibar na wanaotokea Dar es Salaam, Shaaban Kondo (Mbagala Scalet Academy),  Ramadhani Kipicha (Buza) na Shaaban Said (Boom FC ya Ilala).

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC