Klabu ya Young Africans imetangaza kumrejesha mtaalamu wa tiba na viungo bwana Youssef Ammar ambaye hapo awali aliondoka kwenye klabu na nafasi yake kuchukuliwa na Sekhwela Seroto raia wa Afrika Kusini. Youssef Ammar kutoka Tunisia.
Ni mtaalamu na mbobevu mkubwa kwenye masuala mazima ya tiba kwa wachezaji hivyo kurejea kwake klabuni kutaongeza uimara kwenye afya za wachezaji na kuwaepusha na majeraha ya mara kwa mara. Ni mbobevu.
Katika hatua hiyo hiyo, Young Africans pia imemtambulisha mtaalamu wa video (Video Analyst), Thulani Thekiso ambaye ni raia wa Afrika Kusini.
Mtaalamu huyu wa kuchambua video ambaye ametokea kwenye klabu ya Cape Town City ya Afrika kusini amekuja kuchukua nafasi ya Mpho Maruping ambaye ametimka klabuni hivi karibuni.
Mwisho kabisa mabingwa Yanga wamemtambulisha kocha wa makipa aitwaye Majdi Mnasria kutoka Tunisia.
Kocha huyu mwenye uwezo mkubwa wa kuwafundisha walinda milango ametua Yanga akitokea kwenye klabu ya Olympique Akbou ya Algeria.