Kenya, Angola nguvu sawa

WENYEJI, Kenya ‘Harambee Stars’ wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Angola ‘Palancas Negras’ katika mchezo wa Kundi A Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 leo Uwanja wa Moi International Sports Centre, Nairobi.

Mshambuliaji wa Petro Luanda, Jó Paciência alianza kuifungia bao Angola dakika ya saba, kabla ya kiungo mshambuliaji wa Gor Mahia kuisawazishia Kenya dakika ya 12 kwa penalti.

Mchezo mwingine wa Kundi A leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ‘The Leopards’ imeshinda 2-0 dhidi ya Zambia Chipolopolo’ Uwanja wa Taifa wa Nyayo hapo hapo Nairobi.

Mabao ya DR Kongo yamefungwa na  winga wa kushoto wa FC Aigles RDC, Ibrahim Matobo Mubalu dakika ya 51 na mshambuliaji wa DR Congo
FC Saint Eloi Lupopo, Malanga Horso Mwaku dakia ya 71. 

Baada ya mechi za leo Kenya inapanda kileleni ikifikisha pointi nne katika mchezo wa pili na kuishushia nafasi ya pili  Morocco inayobaki na pointi tatu za mechi moja.

DRC inaenda nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu pia baada ya kucheza mechi mbili, wakati Zambia ambayo leo imecheza mechi ya kwanza inaanzia mkiani.