Yanga yapindua meza kwa Tshabalala

Imefahamika kwamba Yanga SC imefanya umafia mkubwa baada ya kumsainisha mkataba mlinzi wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein Tshabalala.

Haikuwa rahisi kwa mchezaji kuachana na timu ambayo yeye ndio nahodha na kwenda timu ambayo ni ngumu kupata unahodha mbele ya kapteni Beka na mwenzie Job,

Haikuwa rahisi kwa Yanga kumchukua mchezaji tegemeo kwenye safu ya ulinzi pale Msimbazi,

Ila pongezi za dhati kwa wakala wa mchezaji, ambae ndiye wakala wa Beka Mwamnyeto na Kibu Denis, kwa kulifanikisha dili hili,

Pongezi za dhati kwa Injinia Hersi na GSM kwa kuhakikisha ndoto za Wanayanga kumuona 'Zimbwe Jr' akujiunga na klabu yao pendwa zikitimia.

Tayari Tshabalala ameshamaliza mkataba wake na Simba hivyo kuhusishwa kwake na Yanga ni dalili njema kwa Wanajangwani hao wanaotaka kutwaa ubingwa kwa mara nyingine ya tano msimu ujao.