Yanga yamtambulisha mbaya wake

WINGA Offen Francis Chikola (26) amejiunga na klabu ya Yanga SC akitokea Tabora United ya Tabora zote za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Jioni hii Yanga kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imeposti Picha Rais wake, Hersi Ally Said akiwa na Chikola na kuambatanisha na ujumbe; Left footer magician Offen Chikola is green and yellow’ kumaanisha mchezaji huyo anayetumia mguu wa kushoto amejiunga na timu hiyo inayotumia jezi za kijani na njano.

Huyo anakuwa mchezaji wa pili tu mpya na wa kwanza mzawa Yanga kuelekea msimu ujao baada ya kiungo wa Kimataifa wa Guinea, Balla Mousa Conte aliyesajiliwa kutoka CS Sfaxien ya Tunisia.

Offen Francis Chikola aliibukia Geita Gold msimu wake 2022-2023 na baada ya timu hiyo kuteremka daraja akahamia Tabora United msimu wa 2024-2025.