Kiungo mahiri kutoka Guinea, Moussa Balla Conte leo ametambulishwa rasmi kuwa Mchezaji mpya wa Klabu ya Yanga SC akitokea CS Sfaxien ya Tunisia ambapo Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo Yanga SC imethibitisha kuipata saini ya kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kupiga pasi za mwisho na kusaidia safu ya ulinzi na ushambuliaji hatua inayowapa mashabiki matumaini mapya kuelekea msimu ujao.
Awali usajili wa Conte uliibua sintofahamu kubwa huku ripoti zikimhusisha pia na mahasimu wao wa jadi Simba SC ambapo ilidaiwa alikuwa karibu kutua Msimbazi ambapo hata hivyo Yanga SC imeweka mambo wazi leo kwa kumtambulisha rasmi ikithibitisha kuwa huduma ya kiungo huyo sasa ni mali ya Wananchi kuelekea kampeni za ndani na Afrika msimu huu.