Mchambuzi wa soka hapa nchini Prince Hoza amesema timu ya Yanga SC itaendelea kutamba mwenye soka la Tanzania, na msimu ujao itatwaa ubingwa wa Tanzania bara.
Akizungumza katika kipindi cha michezo cha Ngome ya Michezo kinachorushwa na redio ya Classic FM 103.3, amedai kwamba Yanga ina kikosi kizuri na haoni kwamba Simba itaweza kubadili timu yake na kuipiku Yanga.
Pia Hoza amedai kwamba Yanga itachukua nafasi ya kwanza huku Simba inaweza kushika nafasi ya pili, lakini ushindani kwenye ligi ya msimu ujao utakuwa mkubwa kutokana na ujio wa makocha Florent Ibenge wa Azam FC na Miguel Gamondi wa Singida Black Stars.