Wadau wamkataa nyota mpya Simba toka Police ya Kenya

Mohamed Babajer ni mchezaji mzuri wa kiwango chake lakini kwa mahitaji timu kubwa za Tanzania ni ngumu kufanya usajili wa wachezaji/ mchezaji kutoka kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kuamini moja kwa moja kutoa ubora wa juu.

Sioni nafasi kubwa ya mchezaji kutoka Africa Mashariki kuja kucheza Simba au Yanga Sc kwa ubora wa juu Katika nyakati hizi.

Simba na Yanga Sc soko lao kubwa kimekua magharibi mwa Africa kutafuta wachezaji.

Ikitokea Simba Sc imesajili huyu kiungo mshambuliaji wa police Kenya basi itakua kamari kubwa sana kwao wamecheza wakitegemea malipo yasiyo na uhakika.