Taarifa kutoka katika vyanzo vyangu vya nje ya nchi ni kwamba Violeth Nicholus atajiunga na klabu ya Masar FC ya nchini Misri.
Violeth atajiunga na Mtanzania mwenzake Hasnath Ubamba ambaye pia yupo katika klabu hiyo tangu misimu miwili nyuma.
Hivyo Violeth pamoja na Hasnath watajeza klabu bingwa wanawake ukanda wa UNAF.
Violeth ni moja ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana na amehudumu kwa mafanikio makubwa Simba Queens akiwa kama mchezaji,kapteni msaidizi na baadae kapteni mkuu.
Vioileth ni moja ya wachezaji wanaosimamiwa na agency ya LTA AGENCY inayomsimamia mchezaji Aisha Masaka,Clara Luvanga na Asha Omary kwa hapa Tanzania.