Timu 5 Afrika kuanzia raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa

Timu za Simba SC, Al Ahly, Esperance, Mamelodi Sundowns na RS Berkane hazitaanzia hatua za awali kwenye michuano ya CAF Champions League msimu wa 2025/26.

Timu hizo pia zitapokea kiasi cha pesa kutoka CAF kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata za michuano hiyo.

“Baada ya kufanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe, tumekubaliana kuanzia msimu wa 2025/2026, vilabu vyote ambavyo vimeondolewa hatua za awali za mashindano ya CAF sasa vitapokea Dola 100,000 kama fedha za kujiandaa kutoka CAF”.

“Huu ni uboreshaji mkubwa kutoka kiasi cha awali cha Dola 50,000 ambacho kilianzishwa msimu uliopita tu kufuatia msimu wa kwanza ya majadiliano ya ACA na CA. Kabla ya hapo vilabu vilivyoondolewa katika hatua za awali hazikuwa zinapokea chochote licha ya rasilimali muhimu na juhudi kubwa wanazochukua kushiriki katika soka la Afrika”.

Eng. Hersi Said (@caamil_88 ) Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu Afrika (ACA).