Simba yamzuia Ahoua kwenda Al Ahli Tripoli

Klabu ya Simba SC imekataa ofa rasmi kutoka Al Ahli Tripoli ikihitaji saini ya kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua (23) katika dirisha hili la uhamisho

Simba SC imesema haitamuachia Jean Charles Ahoua katika dirisha hili kubwa la usajili kuelekea msimu ujao na hii inakuwa ofa ya pili kwa Simba SC kuikataa kutoka Al Ahli Tripoli baada ya ofa ya kukataliwa ya mwezi January