Sheria Ngowi aachana na Yanga

Mbunifu wa jezi za Yanga SC, Sheria Ngowi inasemekana ameachana na klabu hiyo.

Taarifa zandani ambapo Mambo Uwanjani Blog inazipata zinasema mbunifu huyo amemaliza mkataba wake na Yanga na ameamua kutoendelea na kazi nyingine za klabu hiyo

Yanga wako mazungumzo na moja ya kampuni kubwa duniani ya kuzalisha vifaa vya michezo ili kuingia makubaliano ya kuzalisha jezi za msimu ujao.

Baada ya Sheria Ngowi kuondoka,Yanga wanataka kuja na kampuni kubwa yenye ubunifu mkubwa zaidi.