Rayon Sports waenda kujifunga kwa Yanga

UONGOZI wa Klabu ya Rayon Sport ya Rwanda ukiongozwa na Rais wake, Twagirayezu Thaddée umefanya ziara kwenye Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani, Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kwenye mfumo wa Mabadiliko ya Uendeshaji ya mabingwa hao wa Tanzania.