PSG yatinga nusu fainali

PSG wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la dunia la Vilabu baada ya kuwaondoa Bayern Munich wakiwachakaza kwa magoli 2-0 licha ya kuwa pungufu kwa wachezaji 2 kuonyeshwa kadi nyekundu,

Desire Duoe alitangulia kupata goli la kwanza dakika ya 78 goli lililodumu hadi dakika ya 97, Osmane Dembele akikandamiza msumari wa mwisho na kuwahakikishia Bayern uhakika wa Kurejea Nchini kwao Ujerumani.

PSG sasa watakutana na Mshindi kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund mchezo utakaopigwa kuanzia majira ya saa 5:00 usiku

FT: PSG 2-0 Bayern Munich
78’ Doue D.
83’ Pacho W. ♦️
90+2’ Hernandez L ♦️
90+7’ Dembele O.