Olivia Smith aweka rekodi soka la wanawake, avuna bilioni 3 za kibongo

Mshambuliaji wa Canada Olivia Smith ameweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi kusajiliwa katika historia ya soka la wanawake baada ya kukamilisha uhamisho wa kutoka Liverpool kwenda Arsenal wenye thamani ya pauni milioni 1 ambayo ni sawa na bilioni 3.497 kwa fedha za Tanzania.

Uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 unavunja rekodi iliyowekwa na Chelsea Januari 2025 walipomsajili beki wa Marekani Naomi Girma kutoka katika klabu ya San Diego Wave kwa ada ya Pauni laki 9 ambayo ni sawa na bilioni 3.147 kwa fedha za Tanzania

Olivia Smith alijiunga na Liverpool 2024 akitokea katika klabu ya Sporting CP ya Ureno akifunga mabao 7 katika michezo 20 ya ligi kuu aliyocheza ndani ya klabu hiyo na sasa amesaini mkataba wa miaka minne na Arsenal ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.