Mtazamo wa Hans Raphael kuhusu kauli ya MO Dewji

Binafsi nimemsikiliza Tajiri ila sıjaona utofauti wa kile alichoongea msimu uliopita na leo.

Mo anasema ametoa zaidi ya Tsh 80b,inawezekana ni kweli Ila atwambie na Yeye Simba imemtengenezea kiasi gani?….maana kila mwaka anatumia Brand ya Simba kutangaza bidhaa zake.

2. Mo amesema kila mwaka anatoa hela ya usajili ila mambo yamezidi kuwa yale yale kila mwaka Simba wanasajili Wachezaji 17 na mwisho wa Msimu wanakata 14 je Mo haoni pale Simba kuna shida ya utendaji? Kwani asiwaondoe viongozi wote wanaosajili…..? na kuajiri watu wapya wa mpira kama (Technical Director na Drector of football) ili wasimamie vizuri project na Pesa zake? Kwanini ameendelea kuwakumbatia viongozi wale wale ambao kila msimu wanafuja pesa zake kwa kusajili Wachezaji wa kawaida?

Binafsi nadhani hakuna tajiri mjinga ambae kila mwaka atakubali kupoteza hela Yake Kama hapati faida……Mo amekomaa na Simba coz anapata faida,biashara zake zinaenda,Simba ni Brand kubwa ambayo kila tajiri nchini anatamani kuitumia leo asitufanye sisi kama watoto😄

Ifike Muda matamko yakome,vitendo viongee,Simba kabla ya kupata hela ya Mo wanahitaji mfumo mpya wa katiba na viongozi Ila hawa wa Sasa sioni wakifanya Jambo