Mkude aililia Yanga

Ni kama analia kuondoka kwake kwenye kikosi cha Yanga, kiungo mkabaji Jonas Mkude ameonesha masikitiko yake baada ya kutengana na wachezaji wenzake wa Yanga.

Mkude ameachwa kwenye kikosi hicho hicho na tayari ametajwa kujiunga na Singida Black Stars, ameandika katika ukurasa wake.

"Ni uchungu kiasi gani Mimi kutengana na familia hii ya kijani na njano nimeishi katika familia hii Bora na yenye upendo wa thati mtaishi ndani ya moto wangu milele nawapenda sana shabiki zangu nawapenda sana wananchi niwatakie Kila la kheri"