Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC, Kibu Denis , hatoshiriki michuano ya CHAN itakayoanza kuchezwa mwezi wa Agosti katika viwanja vitatu kwenye Nchi za Africa mashariki Yani Tanzania, Uganda na Kenya.
Kocha wa timu ya Taifa Start Hemed Morocco, tayari amemuondoa winga huyo kwenye mipango yake, kwasababu Kibu Denis yupo Nchini Marekani kufanya majaribio katika moja ya Klabu ambayo anatamani kucheza soka la kulipwa huko.
Kibu Denis tayari ameshaanza kupambania ndoto yake huko Merekani na upo uwezekano mdogo sana WA winga huyo Kusalia katika Klabu ya Simba SC msimu ujao wa Mashindano yote ambayo Simba SC watashiriko.