Julien Chevalier kocha mpya Yanga


Baada ya tetesi kuhusu kuondoka kwa kocha Miloud Hamdi ndani ya kikosi cha Yanga kuongezeka kila uchao, Unaambiwa huyu jamaa ndio haswa analengwa na mabingwa hao wa Tanzania ‘Yanga’ kuja kurithi mikoba ya Mzee wetu Miloud Hamdi baada ya kuondoka. Superb!
.
.
Julien Chevalier ni moja ya makocha bora sana barani Afrika kwasasa.. nadhani kama Yanga watafanikiwa kumpata huyu jamaa watakuwa wamelamba dume kwa asilimia kubwa sana. Itoshe kusema kuwa, hiki wanacho kifanya Yanga ni sawa na kumuondoa ‘Bartazar’ na kumleta ‘P-Diddy’ tabu iko pale pale. So sad! .
.
.
Nakumbusha tu, huyu jamaa (Julien Chevalier) ndio alitambulisha ubora wa watu kama Pacome zouzoua, Stephane KI AZIZ, Aubin Kramo n.k katika ulimwengu wa mpira. Nadhani katika kipindi ambacho wanasimba ‘Makolo’ watalia na kusaga meno hadharani, basi ni kipindi ambacho huyu mwamba atafanikiwa kujiunga na Yanga..